Home » » JELA MIAKA MITATU KWA KUJIFANYA AFISA USALAMA WA TAIFA‏

JELA MIAKA MITATU KWA KUJIFANYA AFISA USALAMA WA TAIFA‏


Na Walter Mguluchma-Blogs za Mikoa
Mpanda
Mahakama ya Hakimu   mkazi  ya Wilaya  ya  Mpanda Mkoa wa Katavi  imemhukumu Shaban juma maarufu Mzigaba ( 31) mkzazi wa mtaa  wa Nsemulwa kichangani  mjini hapa  kifungo  cha  miaka  mitatu  jela  kwa  kosa   la kujifanya  afisa usama wa Taifa
Hukumu hiyo  ilitolewa  na Hakimu  mkazi  mfawidhi  wa  mahama  ya wilaya  ya Mpanda Chiganga  Tengwa  na kuguza  hisia  za watu wengi  wa  Mji wa Mpanda na vitongoji  vyake
Awali mwendesha mashitaka wa  jeshi la polisi Razaro Masembo alidai  kuwa  mshitakiwa alitenda  kosa  hilo  katika tarehe tofauti   hapo Aprili  mwaka jana
Alidai  kuwa Shabani  katika  kipindi  hicho  aliweza kujipatia  kiasi  cha   fedha  shilingi  315 000  baada ya  kuwadanganya watu   kuwa  yeye ni  afisa  ulama wa  Tajfa  alitumwa na idara  hiyo  kuorodhesha  majina ya watu  wanao  taka  ajira   ya utumishi  katika  idara  ya TAKUKURU na idara ya usalama wa Taifa
Mshitakiwa baada ya  kuwaorodhesha  majina ya watu hao  aliweza  kuwadanganya wampe  pesa  ili  aweze  kuwapatia nafasi  hizo  za kazi na  ndipo  alipo weza  kupatiwa  na watu hao  kiasi hiccho  cha pesa
Mwandesha mashitaka Masembo  aliileza mahakama  mshitakiwa  alikamatwa  baada  ya watu hao  walio  kuwa wamempa  pesa  kuona muda  umekuwa mwingi  huku  hawaoni kilicho  kuwa kinaendelea  kuhusiana na ajira zao
Alisema watu  hao  ndipo walipo amua kwenda  kutowa  taarifa  kwenye jeshi la polisi wilayani Mpanda  na ndipo  walipo anza  msako na kufanikiwa  kumkamata  mshitakiwa Shabani
Alielezakuwa  miongoni mwa watu  walio danganywa na  mshitakiwa  ni watoto  wa watumishi wa idara mbambali   wa serikali  wa wilaya  hii pamoja  na jeshi  la polisi
Hakimu Chiganga  baada ya kusikiliza  maelezo  ya pande  mbili hizo  za mashitaka  na mshitakiwa  aliridhika na  na  ushahidi   ulio tolewa mahamani hapo  na ndipo  alipo  alipo mtaka mshitakiwa  ajitetee  baada ya mahakama  kumwona  ana hatia
Mshitakiwa  Shaban   katika utetezi wake  aliiomba  mahakama imwachie  huru  kwa kile alicho  kidai kuwa  ushahidi ulio tolewa  dhidi yake  ulikuwa hauna ukweli wowote bali wamemsingizia tuu
Hakimu  Chiganga  aliiambia  mahakama  kuwa  mshitakiwa  amevunja  sheria  ya kifungu cha sheri ya Nchi  namba 100 B  cha kanuni  ya adhabu   cha marekebisho  ya sheria  ya mwaka 2002
Hivyo mahakama  ya  Hakimu  mkazi  ya wilaya ya  hiyo  imemtia hatiani  Shaban Juma imemhukumu kifungo    cha kutumikia  jela miaka  mitatu  ili iwe fundisho kwa watu wengine  wanye tabia ya kujifanya kuwa watumishi wa Serikali
Shaban  baada ya kusomewa   hukumu  hiyo  aliiomba mahakama  impatie  nakala ya hukumu  iliaweze kwenda nayo  gerezani  ombi  ambalo lilitekelezwa na Hakimu Chiganga kwa kumpatia  nakala yake hiyo ya hukumu

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa