Na Walter Mguluchuma,-Blogs za Mikoa
Mpanda- Katavi
Mtu mmoja amekufa hapo hapo na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kugonga mti.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Joseph Myovela amemtaja aliyefariki dunia kwenye ajali hiyo kuwa ni Edes Robart (31) mkazi wa mtaa wa Kawajense mjini hapa.
Ajali hiyo ilitokea hapo jana majira ya saa nne na robo usiku katika eneo la shule ya msingi msakila na kuhusisha pikipiki yenye namba za usajiri T 340 BJK.
Kaimu kamanda wa polisi alimtaja aliyejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo kuwa ni Askari Polisi wa kikosi cha mpanda G 4772 PC Fedrick ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha pikipiki hiyo na amelazwa katika hospitali ya wilaya ya mpanda huku hari yake ikiwa mbaya.
Alisema chanzo cha ajali hiyo kilitokana na mwendokasi wa mwendehaji wa pikipiki hiyo.
Alieleza kuwa marehemu Edes alifariki kutokana na kupatwa na majeraha kichwani baada ya kutovaa kofia kichwani hali iliyopelekea marehemu huyo apasuke kichwa.
Jeshi la polisi mkoani Katavi limetowa wito kwa watumiaji wa pikipiki kufuata sheria za usalama barabarani na kuhakikisha mwendesha pikipiki na abiria wake wote wanavaa kofia.
Hii ni ajali ya pili kutokea kwa kipindi cha siku mbili katika mji wa mpanda ambapo katika tukio jingine watu wane walinusulika kifo baada ya gari lao dogo aina ya NOWA kugongana na Roli aina ya Scania katika eneo la benki ya CRDB mjini hapa.
0 comments:
Post a Comment