Na Walter Mguluchuma,Mpanda.
UMOJA wa Wazee wa mkoa wa Katavi wamefanya mkutano wa mashauriano na taasisi za kifedha wenye lengo na kuboresha masilahi ya wazee,ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wazee kuwa na dhamana ya kupata mikopo katika benki mbalimbali hapa nchini,pamoja na taasisi nyingine za kifedha pamoja na kuanzisha mfuko wao.
Aidha mkutano huo wa mashauriano baina ya wazee wa baadhi ya watendaji wa taasisi za kifedha ikiwemo banki ya CRDB,Benki ya NMB ulifanyika katika ukumbi wa Super City uliopo mjini Mpanda katika mkoa wa katavi ambapo pia mkutano huo Uliwashirikisha watendaji wa halmashauri za mji na wilaya.
Hata hivyo katika mkutano huo Wazee kwa kauli waliiomba serikari kuwaingiza wazee katika agenda ya mipango ya maendeleo kuanzia ngazi za kijiji hadi taifa,kwa lengo la kuboresha hali za wazee ikiwa ni pamoja na kuwaingiza katika mipango itakayowawezesha kupata mikopo katika taasisi za kifedha.
Hata hivyo wazee hao pia walilalamikia sera za mabenki hapa nchini za kutowaruhusu wazee kuwakopesha mikopo ambayo ingeweza kuwasaidia kujikimu kwenye maisha yao.
Kufuatia kauli hizo zilizotolewa na wazee hao ilimlazimu Meneja wa benki ya CRDB tawi la Mpanda Selemani Mbazi kuwaeleza wazee hao wakati akiwasilisha maada yake kuwa utaratibu uliopo wa mabenki hauna utaratibu wa kuwakopesha wazee wote wenye umri wa kuanzia miaka 63.
Mbazi aliwashauri wazee hao kuweka utaratibu wa kuunda vikundi ili waweze kupata mikopo kwani watakuwa wameweza kutiza mashariti ya kupewa mikopo.
Aidha wazee hao pia walipata fursa ya kujadili changamoto zinazowakabili wazee hapa nchini kuwa ni pamoja na wazee kutokuwa na wawakilishi katika vikao vya maendeleo pamoja na vile vya maamuzi.
Hata hivyo wazee hao walisema kuwa pia kutokana na hali yao ya kiumri wamekuwa wakikabiliwa na maradhi mbalimbali yatokanayo na uzee huku kukiwa na tatizo la hospitali,zahanati na vituo vya afya kutokuwa na madaktari waliobobea katika kutoa huduma za matibabu kwa wazee huku sera ya huduma za tiba bure kwa wazee zikishindwa kutekelezeka katika hospitali na vituo vingi ya afya kutokana na ukosefu wa dawa wa mara kwa mara.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa mtandao wa mashirika ya wazee Tanzania (Top) Wilison Karesa alisema kwenye mkutano huo kuwa idadi ya wazee hapa nchini kwa sasa imefikia wazee milioni mbili na ifikapo mwaka 2050 watakuwa wamefika asilimia 10 ya wantanzania wote hapa nchini.
Alisema pamoja na wazee kubeba mizigo mizito bado umuhimu wao hauja tambuliwa kwenye jamii na serikarini kwa ujumla.
Miongoni mwa mizigo wanayo ibeba wazee ni kutunza yatima ambapo asilimia 70 wanatunzwa na wazee na waathirika wa magonjwa mbalimbali wapatao asilimia 80 wana tunzwa na wazee
0 comments:
Post a Comment