Home » » NEWS ALERT:NDEGE YA TANAPA YAANGUKA RUBANI ANUSURIKA KIFO

NEWS ALERT:NDEGE YA TANAPA YAANGUKA RUBANI ANUSURIKA KIFO









Ndege yashirika la hifadhi la taifa (TANAPA) yenye namba za usajili 5H-PZS aina ya C182 ikiwa imeanguka katika eneo la nsemulwa mjini Mpanda muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa mjini mpanda ikiwa inaendeshwa na rubani Adam kajwa aliepata majeraha sehemu ya uso. Ajali hiyo imetokea majira ya saa 10:55 jioni wakati ndege hiyo ikielekea hifadhi ya taifa ya katavi wilayani mlele mkoa wa katavi. picha na walter mguluchuma
*****

na walter mguluchuma,mpanda     
Ndege ya hifadhi ya taifa ya TANAPA   imepata  ajari  ya kuanguka  wilayani Mpanda mkoa wa Katavi    na rubani wa ndege hiyo  kunusurika  kifo  baada ya kupata majeruhi
Meneja wa uwanja wa ndege wa Mpanda  Mahamud Muhamed  alisema  ajari  hiyo  ilitokea jana  majila ya  saa 10  na dakika 55 jioni  katika  kijiji  cha Nsemlwa   wilayani hapo
ndege hiyo  iliyo  anguka  ilikuwa namba za usajiri  5H--  FZS aina  ya  C182  ndege ndogo  ya abiria  mari ya hifadhi ya taifa ya  TANAPA iliyo  kuwa ikiendeshwa na rubani   Adamu  Athumani  Kajwaa yenye uwezo  wa kuchukua abiria  wane
Muhamed  alieleza kuwa  ndege  hiyo   ilikuwa imetoka  katika uwanja wa ndege wa mpanda     ikielekea  katika hifadhi ya wanyama pori  ya Katavi   wilayani Mlele
  Ajari  hiyo  ilitokea   umbali wa  kilimeta  moja na  nusu  kutoka uwanja wa ndege wa Mpanda  mara  baada  ya  kuondoka  katika uwanja huo ambapo imeharibika sana sehemu ya bawa lake na upande wa injini.
 Meneja wa uwanja  huo wa ndege  alisema  taarifa za awali   zinaonyesha  chanzo   cha ajari  hiyo  kilitokana na    njini  ya ndege  hiyo  kufeli wakati ikiwa angani
Rubani wa ndege hiyo   alipata msaada  wa  wa kuokokewa na  wananchi  waliokuwa  wakifanya  shughuli  za  kilimo  kwenye  mashamba  yao
 Mmoja wa  walio shuhudi tukio  hilo  Credo Mwanisenga   alieleza  kuwa wakati   akiwa  anafanya shughuli  zake  za kilimo  ghafla  aliona  ndege  iliyo  kuwa  angani  ikizimika  na kisha  baada ya  muda  mfupi   ikaanguka   jirani  na mti wa mwembe
Na mara  walifika katika eneo hilo  kwa lengo la kutowa msaada  hata hivyo  iliwachukuwa muda  kuanza kutowa msaada  kwa  rubani huyo  aliye kuwa ndani ya ndege  peke yake  kutokana  na eneo hilo kuwa na nyuki wengi  ambao walianza kuwashambulia waokoaji hao
Hata hivyo  waliewza  kufanikiwa kumtoa  rubani  huyo   huku akiwa  amepata  majeruhi makubwa sehemu ya  uso  wake  na maumivu  sehemu ya kifua  huku akiwa anakohoa damu  na  aliewza kukimbizwa  haraka katika hosptali ya wilaya ya mpanda baada ya kupata  msaada wa gari la meneja wa uwanja wa ndege aliye fika kwenye eneo   la tukio
Rubani   wa ndege hiyo aliweza kupatiwa matibabu  katika hospitali ya wilaya yam panda  kwa kushonwa nyuzi  nane katika  paji la uso wake  na kasha aripewa ruhusa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa