MIZENGO PINDA ATAKA WANA CCM KUJIEPUSHA NA MANENO YA UCHOCHEZI

Na Munir Shemweta, MLELE  

Waziri Mkuu Mstaafu ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mhe. Mizengo Pinda amewataka wanachama CCM wanaotaka kugombea nafasi yoyote kujiepusha na maneno ya uchochezi yanayoweza kuharibu mahusiano baina yao.

 

Pinda amesema hayo tarehe 20 Julai 2024 wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa CCM wakiwemo madiwani, viongozi wa kata pamoja na wazee katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.

 

Amesema, kwa yoyote anayetaka kugombea nafasi ya uongozi ni vizuri akawa muangalifu na maneno ya uchochezi aliyoyaeleza kuwa, wakati mwingine yanaweza kumletea tabu wakati haipo.

 

"Chonde chonde sana usije ukaingia kwenye ugonjwa, unakaa unakuzungusha kicwa kwa sababu kuna mtu kaja kukuambia eeh kuma mtu fulani anakusema vibaya sasa hujathibitisha unaanza kutembea nayo na wewe usiende hivyo kwenye siasa hatuendi hivyo" amesema Mizengo Pinda

 

Amewataka wanapopelekewa maneno kuyapokea na kutulia huku wakijaribu kuyachunguza ili kuona ukweli au uongo kwa kile wanachoambiwa na kuweka wazi kuwa, wengi huponzwa na maneno ambapo amesisitiza, wana CCM kujaribu kupunguza maneno ya uchochezi yatakayosababisha kukwaruzana pasipo sababu ya msingi.

 

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kavuu ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ameeleza kuwa, hali ya kiasiasa ndani ya jimbo lake iko shwari na amekuwa akifanya vikao vya mara kwa mara kwa wananchi wa rika zote kupitia kata za jimbo hilo.

 

Hata hivyo, Mbunge huyo ameweka wazi kuwa, wakati mwingine kwa namna moja ama nyingine amashindwa kumfikia kila mwananchi kwenye jimbo hilo kutokana na idadi kubwa ya wakazi wake aliyoieleza kwamba imekuwa ikiongezeka siku hadi siku.

 

Amebainisha kuwa, kupitia wizara yake ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wako mbioni  kuweka mipango ya  matumizi bora ya ardhi kwa kila kijiji ila  wanachi wapate hati milki za ardhi na kuweza kuzitumia kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuchukulia mikopo benki.

 


 

 

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan azindua Vihenge na Maghala ya Kisasa kuhifadhia Nafaka ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi wa Chakula (NFRA) Mpanda mkoani Katavi


. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo wakati alipotembelea sehemu ya mfumo wa upimaji Nafaka kabla ya kuzindua mfumo ununuzi wa nafaka kwa msimu wa 2024-2025, Mpanda Mkoani Katavi tarehe 14 Julai, 2024.


Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi iliyopo Mpanda katika muendelezo wa Ziara yake ya kikazi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu akizungumza na Wananchi mara baada ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi iliyopo Mpanda katika Muendelezo wa Ziara yake ya Kikazi mkoani humo tarehe 14 Julai, 2024.


 

RAIS DKT. SAMIA AIPA HONGERA NSSF

RAIS DKT. SAMIA AIPA HONGERA NSSF
Na MWANDISHI WETU,
Katavi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi kwa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) baada ya kuelezwa mafanikio mbalimbali ambayo NSSF imeyapata katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake.

Pongezi hizo alizitoa tarehe 13 Julai, 2024 wakati alipotembelea banda la NSSF kwenye kilele cha Wiki ya Wazazi iliyofanyika Mjini Mpanda Mkoani Katavi. NSSF imeshiriki katika kutoa elimu ya hifadhi ya jamii katika maadhimisho hayo kwani Jumuiya ya Wazazi ni mojawapo ya wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii ( NSSF).

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Bi. Lulu Mengele amesema NSSF inamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia kwa namna alivyofungua nchi, ambapo wafanyakazi kwenye sekta binafsi wakiwemo wale wa viwandani  wameongezeka na kuiwezesha NSSF kupata wanachama wapya.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tunakupongeza kwa kazi kubwa unayoifanya, umefungua fursa mbalimbali ambapo wakati unaingia madarakani mwaka 2021 thamani ya NSSF ilikuwa ni Shilingi Trilioni 4.8 lakini sasa imepanda kwa juhudi kubwa ambazo umefanya tumefikia Trilioni 8.5,” amesema Bi. Mengele.

Amesema NSSF inaendelea kuboresha mifumo yake ya TEHAMA ambapo hivi sasa mwajiri anaweza kumwandikisha na kuwachangia wafanyakazi wake kulekule walipo na pia mwanachama anaweza kuangalia taarifa zake mbalimbali bila ya kulazimika kufika katika ofisi za NSSF na kwa hatua hiyo imerahisisha huduma kwa wanachama.

Akizungumzia ushiriki wa NSSF katika Kilele cha Wiki ya Wazazi, Bi. Lulu alimueleza Mhe. Rais Dkt. Samia kuwa NSSF imeshiriki Maonesho yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi kwa kuwa wafanyakazi wa Jumuiya ya Wazazi ni wanachama wa NSSF kama zilivyo Jumuiya nyingine za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Bi. Lulu amesema wametumia maonesho hayo kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wanachama waliotembelea kwenye Banda hilo, matumizi ya mifumo kwa waajiriwa na waajiri ambapo wakiwa popote wanaweza wakapata taarifa zao za michango na kuwasilisha michango bila kulazimika kutembelea ofisi za NSSF.

Amesema NSSF inaendelea kufanya vizuri kwa kuweka kipaumbele  cha kuwarahishia huduma wanachama wake.

 

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan afungua Jengo la Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Katavi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati ukiimbwa Wimbo wa Taifa pamoja na ule wa Afrika Mashariki katika viwanja vya Jengo la Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Katavi tarehe 14 Julai, 2024. 


 

 

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan azungumza na Wananchi wa Mpanda katika Kilele cha Wiki ya Wazazi Kitaifa Mkoani Katavi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wananchi wa Mpanda kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika wakati wa Kilele cha Wiki ya Wazazi mkoani Katavi katika Viwanja vya Azimio, Mkoani Katavi tarehe 13 Julai, 2024.

 

Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan ahudhuria Kilele cha Wiki ya Wazazi Kitaifa Mpanda Mkoani Katavi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika wakati wa Kilele cha Wiki ya Wazazi Mpanda mkoani Katavi. Mkutano huo ambao umeandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania ulifanyika katika Viwanja vya Azimio, Mkoani Katavi tarehe 13 Julai, 2024. 


 

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa