Na mwandishi wetu, Katavi
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Abdulrahman Kinana
amewashauri viongozi wa CCM wa ngazi mbalimbali kuwa mfano bora wa
maadili na malezi mema.
Ameeleza
hayo leo Julai 11, 2024 alipofungua Kongamano la Malezi na Maadili
lililondaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama, mjini Mpanda, mkoani
Katavi.
“Sisi
viongozi tunatakiwa kuwa mfano wa maadili na hasa viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi kwa kuepuka mambo yote ambayo yataleta sifa mbaya kwa Chama
au kuleta sifa mbaya kwa wana CCM na viongozi wake.
“Tunawajibu
wa kuyasimamia maaadili, maadili ni mambo yote mema na kueupka mabaya.
Sisi viongozi ndani ya CCM tunatakiwa wakati wote kuwa mfano kwa kauli
zetu na vitendo vyetu kwa maisha yetu yote.Tuwe mfano wa uadilifu, kila
anayekuona uwe tafsri ya maadili, tuwe tafsiri ya sifa za uadilifu,”
ameema.
Kwa
mujibu wa Kinana, CCM imeendelea kuwa chuo cha maadili ndio maana
kumekuwa na Kamati za kusimamia maadili katika ngazi zote kuanzia chini
hadi Taifa.
Amesisitiza
kuwa kauli zinazotolewa na viongozi mbalimbali zinadhihirisha maadili,
kukemea rushwa, mambo yasiyo mema kwa jamii na kuhimiza kujenga undugu,
mshikamano na kusaidiana.
0 comments:
Post a Comment