Sunday, December 23, 2012

Wazee wa Katavi wapewa somo na banki ya CRDB‏


Na Walter Mguluchuma,Mpanda.

UMOJA wa Wazee wa mkoa wa Katavi wamefanya mkutano  wa mashauriano na taasisi za kifedha  wenye lengo  na kuboresha  masilahi ya  wazee,ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wazee kuwa na dhamana ya kupata mikopo katika benki mbalimbali hapa nchini,pamoja na taasisi nyingine za kifedha   pamoja na kuanzisha  mfuko wao.

Aidha mkutano huo wa mashauriano baina ya wazee wa baadhi ya watendaji wa taasisi za kifedha ikiwemo banki ya CRDB,Benki ya NMB ulifanyika katika ukumbi  wa  Super City   uliopo mjini Mpanda   katika mkoa wa katavi  ambapo  pia mkutano huo Uliwashirikisha watendaji  wa  halmashauri  za mji  na wilaya.

 Hata hivyo katika mkutano huo Wazee  kwa kauli waliiomba serikari kuwaingiza wazee  katika  agenda  ya mipango  ya maendeleo  kuanzia ngazi  za   kijiji hadi taifa,kwa lengo la kuboresha  hali za wazee ikiwa ni pamoja na kuwaingiza katika mipango itakayowawezesha kupata mikopo katika taasisi za kifedha.


Hata hivyo wazee hao pia  walilalamikia  sera za mabenki hapa nchini  za kutowaruhusu wazee kuwakopesha mikopo ambayo ingeweza kuwasaidia kujikimu kwenye maisha yao.



Kufuatia kauli hizo zilizotolewa na wazee hao ilimlazimu Meneja wa  benki ya  CRDB tawi la Mpanda   Selemani  Mbazi   kuwaeleza wazee hao wakati akiwasilisha maada yake  kuwa  utaratibu uliopo wa mabenki  hauna utaratibu wa kuwakopesha wazee wote wenye umri wa kuanzia miaka 63.

Mbazi  aliwashauri wazee hao  kuweka utaratibu  wa kuunda  vikundi  ili waweze kupata mikopo   kwani   watakuwa wameweza kutiza mashariti ya kupewa mikopo.


Aidha wazee hao pia walipata fursa ya kujadili changamoto zinazowakabili wazee hapa nchini kuwa  ni pamoja na wazee kutokuwa na wawakilishi katika vikao vya maendeleo pamoja na  vile vya maamuzi.

Hata hivyo wazee hao walisema kuwa pia kutokana na hali  yao ya kiumri wamekuwa wakikabiliwa  na maradhi mbalimbali yatokanayo na uzee   huku kukiwa na tatizo la hospitali,zahanati na vituo  vya afya kutokuwa na madaktari waliobobea katika kutoa huduma za matibabu  kwa wazee huku sera ya huduma za tiba  bure kwa wazee zikishindwa kutekelezeka katika hospitali na vituo vingi ya afya kutokana na ukosefu wa dawa wa mara kwa mara.


Kwa upande wake  Katibu mkuu wa  mtandao wa  mashirika  ya wazee   Tanzania  (Top)   Wilison  Karesa   alisema kwenye mkutano huo  kuwa   idadi  ya wazee  hapa nchini  kwa sasa imefikia   wazee milioni mbili  na ifikapo mwaka 2050  watakuwa wamefika asilimia 10  ya wantanzania wote hapa  nchini.

 Alisema  pamoja na wazee kubeba  mizigo  mizito   bado  umuhimu wao  hauja tambuliwa kwenye  jamii  na serikarini kwa ujumla.

 Miongoni mwa mizigo wanayo ibeba wazee ni kutunza yatima  ambapo asilimia 70  wanatunzwa na wazee na  waathirika wa magonjwa mbalimbali wapatao asilimia  80 wana tunzwa na wazee  

No comments:

Post a Comment