Sunday, December 23, 2012

MWENYEKITI WA BARAZA LA VIJANA MIKOA YA RUKWA NA KATAVI AAHIDI KUKATA RUFAA BAADA YA KUKABIDHIWA BARUA YA KUVULIWA MADARAKA


ZIKIWA zimepita takribani siku tatu  baada cha chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema  Mikoa ya Rukwa na Katavi kutoa tamko kwa vyombo  vya habari la kumvua madaraka Mwenyekiti wa baraza la Vijana wa mikoa hiyo Bw Laurent Mangweshi huku akiwa hajakabidhiwa barua ya kimaandishi inayohusu kuvuliwa madaraka amesem kuwa mara baada ya kukabidhiwa barua yake atakata rufaa kwa lengo la kupata haki yake.

Akizungumza na gazeti hili kwa ya Simu Magweshi’amesema kuwa mpaka sasa swala la kuvuliwa kwangu madaraka nalisikia tu katika vyombo vya habari na wadau wangu wengine lakini nakiri kuwa mpaksa sasa sina barua wala kieelezo chochote kinachoonyesha kuwa nimevuliwa madaraka ndani ya chama na hivyo nasema kuwa taaarifa hizo zilizozagaa mitaani  ni uzushi tu mie bado ni mwenyekiti wa baraza za vijana wa mikoa  ya Rukwa na Katavi alisema Magweshi
.
Alopohojiwa juu ya kuonywa mara kadhaa katika vikao kutokana na utovu wa nidhamu alisema kuwa katika maisha yake hajawahi kuonywa na tangu kujiunga kwake ndani ya chama  cha demokrasia na maendeleo mwaka 2001 hakuna kikao cha Baraza la Uongozi lililokaa na  kufafanua kuwa baraza la Usuruhisho hallina mamlaka ya kutoa adhabu wala kumvua mtu madaraka na kusema kuwa kikao cha mjini Namanyere kilikuwa ni cha baraza la Usuruhishi na si cha barala la uongozi lenye mamlaka.

Hata hivyo Bw Magweshi alihoji  kwanini viongozi hao wamekimbilia katika vyombo vya habari na kutoa Tamko kabla ya kukamilisha taratibu zote za kichama ikiwemo ile ya kuandikiwa barua  na kuongeza kuwa yeye ndiye aliyepaswa kukimbilia katika vyombo vya habari kwa lengo la kutafuta haki yake endapo angekabidhiwa barua na si  viongozi hao.

Alipohojiwa juu ya  hatua gani  atazichukua endapo ataona haki yake haijatendeka ndani ya chama hicho  je  atakuwa na mpango wa kuondoka ndani ya chama hicho na mwelekeo wake  ni chama kipi? Mangweshi alisema kuwa sina mpango wowote wa kuhihama chadema mimi nitafia chadema kwa kuwa chadema  nia yake ni kulikomboa taifa toka katika chama cha mapinduzi na kuleta  mabadiliko ya kweli  na mimi nakuhakikishia kuwa ni Chadema Original  naipenda sana chadema ila siwezi kukubali  kukiaibisha chama changu na wala sina njaa za kuhamahama vyama alisema Magweshi.

Alisema kuwa’nawaheshimu sana viongozi wangu  na nitaendelea kufanya kazi kwa lengo la kukijenga chama  na nasema kuwa hakuna binadamu aliye  mkamilifu kwa asilimia mia moja bali kila binadamu namapungufu yake.

Hata hivyo kufuatia taarifa hiyo ya kutokabidhiwa kwa barua  kwa wakati  mwenyekiti   huyo wa baraza la vijana anayedaiwa kuvuliwa madaraka  kutokana na sababu mbalimbali gazeti hii lilifanikiwa kufanya mahojiano na Katibu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Mikoa ya Rukwa na Katavi Bw Ozem Chapita  ambaye licha  kukiri kucheleweshwa kwa tukio hilo la kumkabidhi barua alifafanua kuwa hali hiyo imetokana na mazingira ya kazi kutoakana  hali ya mwenyekiti huyo kuishi mkoani katavi huko katibu huyo ambaye ni mtendaji  mkuu akiwa anaishi mkoani Rukwa.

Hata Hivyo Chapita alisema kuwa mpaka sasa amekwisha fanya utaratibu wa kusafirisha barua hiyo kwa njia ya Basi  ili iweze kumfikia Magweshi.

No comments:

Post a Comment