na Walter Mguluchuma Mpanda
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi limemuagiza Mkurungnzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha Vijiji vyote ambavyo avikufanya uchaguzi wa viongozi wa jiji na jitongoji vilivyo ongezwa vinafanya uchaguzi huo kabla ya mwezi juni mwakani.
agizi hilo limetolewa na baraza hilo kufuatia ombi lililo tolewa na mbunge wa jimbo la mpanda vijijini moshi kakoso kwenye kikao cha baraza la madiwani kilicho fanyika juzi kwenye ukumbi wa idara ya maji.
Kakoso alilieleza baraza hilo kuwa ipo baadhi ya miradi ya maendeleo kwenye vijiji imesima ma kutokana na maeneo hayo kutokuwa na viongozi wa serikali ya kijiji.
nae diwani wa kata ya mpanda ndogo hamad mapengo aliliambia baraza hilo kuwa kata yake inajumla ya vijiji 9 kati ya hivyo vijiji vitatu havina uongozi wa serikali ya kijiji.
alivitaja jiji hivyo kwenye kata yake ambavyo avina uongozi kuwa ni mnyamasi bugwe na vikonge hari inayo pelekea wakazi wa maeneo hayo wajione kama vile wametengwa.
alisema hari hiyo imesababisha miradi ya maendeleo iliyopelekwa kwenye vijiji hivyo kukosa mtu wa kuisimamia kwani viongozi wa vijiji vya jirani maeneo yao yako mbali na maneo hayo.
kwa upande wake mkurungezi wa halmashauri ya wilaya ya mpanda estomioh chong’ah alisema kuwa tayari wameisha kaa na vyama vya siasa na wamekubaliana kufanya uchuguzi huo mara tuu mvua za masika zitakapo malizika.
katika kikao hicho madiwani walihoji sababu iliyo pelekea kuwafanya viongozi wa vijiji na vitongoji ambao walishiriki kwenye kuwaongoza makarni wa sensa kwenye maeneo kilicho sababisha mpaka sasa kutolipwa malipo yao.
hari ambayo ilimfanya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo amtake afisa mipango wa Halmashauri ajibu hoja hiyo iliyo anzishwa na Diwani wa Kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele.
hata hivyo afisa mipango alieleza kuwa yeye hana majibu ya kutosheleza kwani mratibu aliye kuwa akisimamia zoezi hilo hayupo wilayani hapo kwa sasa.
No comments:
Post a Comment