Home » » TATIZO LA VIJIJI KUKOSA KUWA NA VIONGOZI WA SERIKALI WASABABISHA MIRADI KUSIMAMA

TATIZO LA VIJIJI KUKOSA KUWA NA VIONGOZI WA SERIKALI WASABABISHA MIRADI KUSIMAMA


na Walter  Mguluchuma  Mpanda

Baraza la Madiwani la  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  Mkoa wa Katavi  limemuagiza Mkurungnzi  wa Halmashauri ya Wilaya  hiyo  kuhakikisha  Vijiji vyote ambavyo  avikufanya  uchaguzi  wa  viongozi  wa jiji  na jitongoji  vilivyo  ongezwa  vinafanya uchaguzi  huo  kabla ya mwezi juni mwakani.

 agizi  hilo  limetolewa na  baraza hilo  kufuatia    ombi lililo  tolewa na  mbunge  wa jimbo  la mpanda vijijini  moshi  kakoso  kwenye kikao  cha  baraza la madiwani kilicho  fanyika juzi  kwenye  ukumbi wa  idara ya maji.

Kakoso  alilieleza baraza hilo  kuwa  ipo  baadhi  ya miradi ya maendeleo    kwenye  vijiji  imesima ma  kutokana   na  maeneo  hayo kutokuwa  na viongozi wa serikali ya kijiji.
  
 nae diwani wa kata ya mpanda ndogo  hamad mapengo aliliambia baraza hilo  kuwa kata yake  inajumla ya vijiji  9  kati ya hivyo  vijiji  vitatu  havina    uongozi wa serikali ya kijiji.

 alivitaja jiji hivyo  kwenye kata yake  ambavyo avina uongozi  kuwa ni mnyamasi  bugwe na  vikonge  hari  inayo pelekea wakazi wa maeneo hayo   wajione kama vile wametengwa.

 alisema  hari hiyo  imesababisha     miradi ya maendeleo  iliyopelekwa kwenye   vijiji hivyo  kukosa mtu wa kuisimamia   kwani  viongozi wa vijiji  vya jirani  maeneo yao yako mbali na  maneo hayo.

kwa upande wake mkurungezi wa halmashauri ya wilaya ya mpanda estomioh  chong’ah alisema kuwa tayari wameisha kaa na vyama vya siasa na wamekubaliana kufanya uchuguzi  huo  mara tuu mvua za masika zitakapo malizika.

 katika kikao  hicho   madiwani  walihoji  sababu  iliyo  pelekea  kuwafanya  viongozi wa vijiji  na vitongoji  ambao  walishiriki kwenye  kuwaongoza makarni  wa sensa kwenye maeneo   kilicho  sababisha mpaka sasa kutolipwa  malipo yao.

 hari ambayo  ilimfanya Mkurugenzi wa  Halmashauri  hiyo  amtake  afisa mipango  wa Halmashauri   ajibu  hoja hiyo  iliyo  anzishwa na Diwani wa Kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele.

 hata hivyo  afisa mipango  alieleza kuwa yeye hana majibu ya  kutosheleza   kwani mratibu  aliye kuwa akisimamia zoezi hilo  hayupo   wilayani hapo kwa sasa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa