Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Michael Nzyungu amewapa onyo Maafisa watendaji watatu wa Kata ambao wameshindwa kutekeleza maagizo ya Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo.
Nzyungu alikiambia jana kikao cha Baraza la Madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo kuwa amewandikia barua za onyo maafisa watatu wa watendaji wa Kata ambazo zimeshindwa kutekeleza agizo la Baraza la madiwani walilolitowa la kuwataka watendaji wote wa Kata kuwasilisha taariza za utekelezaji wa shughuli zinazofanywa kwenye Kata zao kila baada ya miezi mitatu.
Alilieleza Baraza hilo kuwa katika Kata kumi na tano zilizopo kwenye Manispaa hiyo watendaji kumi na mbili wameweza kuwasilisha taarifa zao kama ambazovyo baraza la madiwani lilivyo wataka kufanya hivyo lakini kata tatu zimeshindwa kufanya hivyo .
Alizitaja Kata ambazo watendaji wake wameshindwa kuwasilisha taarifa zao za utendaji wa shughuli zinazofanywa kwenye Kata zao za kipindi cha robo tatu ya mwaka kuwa ni maafisa watendaji wa Kata za Majengo , Kasokola na Kakese .
Alisema amelazimika kuwapa onyo maafisa hao watendaji wa Kata kwa kushindw kutekeleza maagizo ya Baraza la madiwani kitu ambacho ni uzembe mkubwa sana kwa mtumishi kushindwa kutekeleza maagizo ya baraza la madiwani .
Nae Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo alisema kuwa maagizo ya Baraza la madiwani ni kitu kikubwa sana hivyo ni lazima yawe yanatekelezwa kadri yanavyo kuwa yametolewa na sivinginevyo .
Na aliwataka wataalamu wote wa Manispaa hiyo kuwahakikisha wanaheshimu vikao vya baraza la madiwani kwa kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani bila kukosa .
Mbogo alilieleza Baraza hilo kuwa hari ya barabara katika Manispaa hiyo zimeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivyo wanawasiliana na wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA ili waweze kuzitengeneza kwani kwa sasa Halmashauri hazihusiki na matengenezo ya barabara.
Aliyataka mashirika yote na taasisi zilizopo katika Manispaa hiyo watii mamalaka na sheria za Serikali za mitaa kwa kufanya usafi kwenye maeneo yao kama ambazo inavyoelekezwa kwani zipo taasisi za umma zimekuwa hazitii sheria.
Diwani wa Kata ya Makanyagio Haidari Sumry kwa upande wake aliliambia baraza hilo la madiwani kuwa msimu wa kilimowa mwaka jana wakulima walichelewa kufikishiwa mbole kwa wakati hari ambayo iliwafanya wakulima wapate hasara ya kuvuna mazao machache hivyo aliiomba kwa mwaka huu wakulima wapatiwe mbole na pembejeo za kilimo kwa wakati .
Aliomba pia ruzuku zinazotolewa kwenye mbolea zitolewe pia kwenye mbegu kwani bei ya mbegu zipo juu sana kwani baadhi ya mbegu kilo moja inauzwa mpaka TSHS 10,000.
Kwa upande wake Diwani wa vitu maalumu Getruda Kaminda aliipongeza Kata ya Kashaulili kwa kuwaza kupunguza kuondoa taka kwa asilimia 85.
Baraza hilo la madiwani kwa kauli moja limempongeza Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga kutokana na jitihada kubwa anayofanya katika manispaa hiyo ya kuwahamasisha wadau mbalimbali ambao wameweza kuchangia katika swala la elimu kwa kujenga madarasa na kuchangia madawati.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment