Shehena za mahindi zikiwa zimerundikana katika kituo cha shirika la reli (TRL) kituo cha Mpanda baada kushindwa kusafirishwa kwenda Mikoa ya kanda ya ziwa kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.
Alhamisi ya wiki iliyopita
wafanya biashara wa mahindi wanaosafirisa mazao hayo waliamua kulala kwenye
mataruma ya reli kuizuia treni ya mizigo iliyokuwa inakwenda kuchukua mahindi
kwenye maghala ya akiba ya chakula cha Taifa yaliyopo karibu na kituo cha reli
cha Mpanda.
Lengo la wafanya
biashara kulala katika mataruma ya reli walikuwa wanalishinikiza shirika la
reli liwasafirishie mazao yao wakihofia kuharibika kwa mvua za msimu wa kilimo
zinazo tegemea kuanza kunyesha mwezi ujao.
Picha na Walter
Mguluchuma
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment