Home » » ALIYEDANGANYWA NA WAGANGA KUMFUFUA MWANAE ALIYEKUFA AHUKUMIWA KULIPA NG'OMBE NA BARAZA LA WAZEE WA KISUKUMA.

ALIYEDANGANYWA NA WAGANGA KUMFUFUA MWANAE ALIYEKUFA AHUKUMIWA KULIPA NG'OMBE NA BARAZA LA WAZEE WA KISUKUMA.

Na Walter Mguluchuma, Katavi Yetu

Wazee wa kimila wa kabila la wasukuma wa kata ya kakese wilayani Mpanda wamemhukumu mwenzao mmoja kulipa ngombe baada ya kukiri kosa la kudanganya na waganga wa jadi kuwa mtoto wake aliyefariki dunia atafufuliwa akiwa hai

Katika tukio hilo ambalo liligusa hisia za watu wengi wilayani mpanda Lumba Mwinamila siku hiyo ya septemba 2 mwaka huu ambayo ilikua siku ya mazishi ya mtoto wake aitwaye Sikitu Mwinamila (40) aliwazuia viongozi wa dini wa dhehebu la AIC na waombolezaji wasimzike mwanae kwani kunashughuli za kimila wanamfanyia mwanae na atatolewa kwenye jeneza na kuwa hai

Kikao hicho cha baraza la wazee wa kabila la wasukuma kilifanyika hapo juzi na kiliwahusisha wajumbe wote wa kata ya kakese kilimtaka mwinamila atoe maelezo yaliyosababisha achukue jukumu la kushirikia na waganga wa jadi kuutoa nje ya sanduku mwili wa marehemu kitendo ambacho ni udhalilishaji wa maiti nanikinyume cha desturi la kabila la wasukuma

Mwinamila katika baraza hilo alilielekeza kuwa yeye binafsi alikuwa na imani kubwa na waganga hao wa jadi kuwa hawawezi kuwa waongo kutokana na mahusiano ya kindugu waliyokuwa nayo kwani katika waganga hao wawili aliowatoa mkoani Shinyanga mmoja alikuwa ni mwanae wa kumzaa na wa pili alikua ni dada yake ambae pia ni shangazi wa marehemu sikitu

Kufuatia maelezo hayo ya mwinamila mbele ya baraza la wazee hao wa kisukuma la kumpa adhabu ya kulipa ngombe mmoja kama utaratibu ambao ulishawekwa wa kabila lao la kisukuma

pia baraza hilo liliamua kumtenga kushirikiana mnae katika masuala ya kijammi mpaka hapo atakapo kuwa amelipa ngombe hiyo na wala haruhusiwi kwenda kuchota maji kwenye kisima au mto wanao tumia watu wa kabila la kisukuma

siku hiyo ya tukio la jumapili mwinamili kwa kushirikiana na waganga hao wawili wa jadi kutoka shinyanga waliutoa mwili wa marehemu ndani ya jeneza kwa kile walichokidai wanamtengenezea dawa ili waweze kumfufua

kitendo ambacho kiliwaudhi watu wengi katika msiba huo hasa pale walipotoa mwili wa marehemu sikitu nje ya uwanja wa nyumba huku akiwa amevaa soksi na suruali huku wakiwa wamemshikilia mikono na wakidai kuwa wanataka kumfufua marehemu huyo tendo ambalo liliwashinda

hali hiyo iliyowafanya waombolezaji waliokuwa hapo msibani wakiuona mwili wa marehemu ukiwa umesimamishwa waliamua kutimua mbio na wengine kupotea njia na wakaja kujikuta wametokea kwenye vijiji vya jirani na wengine kujiktua wameelekea vichakani.

marehemu sikitu alifariki hapo Agosti 30 katika hospitali ya wilaya ya mpanda kutokana na ajali ya pikipiki na kifo chake kilisababishwa na damu nyingi kuvuja kifuani na baba wa mzazi wa marehemu alipopata taarifa ya kifo hicho alizuia mazishi yasifanyike ili wasubirie waganga hao wawili kutoka Shinyanga kwa lengo la kuja kumfufua.

Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa