Home » » POLISI KATAVI KUWACHUKULIA HATUA WATAKAOSHAWISHI VURUGU

POLISI KATAVI KUWACHUKULIA HATUA WATAKAOSHAWISHI VURUGU


Na Walter Mguluchuma, Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limewaonya walimu wote watakaowashinikiza wanafunzi kuandamana na kufanya vurugu kwa kisingizio cha kudai haki zao watachukuliwa hatua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahili Kidavashari alitoa kauli hiyo hapo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu au mwalimu yoyote atakaye bainika kujihusisha na vitendo vya kuwatisha walimu wanaoendelea kuwafundisha wanafunzi kwenye kipindi hiki cha mgomo wa walimu nchini.
Kidavashari alieleza kuwa jeshi la polisi lina wajibu mkubwa wa kusimamia sheria, kulinda raia na mali zao hivyo alishauri kwa wanaotaka kufundisha waendelee kufanya kazi yao na watalindwa kwa mujibu wa sheria.
Nae katibu wa chama cha walimu mkoa wa katavi na rukwa Tweedsmus Zambi alisema mgomo huo wa walimu katika mikoa yake vitaendelea mpaka hapo serikali itakapokaa nao.
Alieleza mgomo huo wa walimu utasitishwa mpaka hapo taratibu zitakapo kamilika kwa meza ya mazungumzo.
Pia alisema mgomo huo unao endelea nchini koto wa walimu ni waarali kwani upo kisheria namba 6 ya mwaka 2004.
Miongoni mwa madai wanayodai walimu ni malipo ya posho ya kufanya kazi kwenye mazingira magumu kwa wale wanao stahili.
Madai yao mengine ni kulipwa posho ya kufundishia kwa walimu  wa hati na sanaa wanaongozewa kwa asilimia 50%
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa