Na Walter mguluchuma
Mpanda-Katavi yetu Blog
Zaidi ya mifugo mia tisa ya ng’ombe imekamatwa wilayani mlele mkoani katavi kwa kipindi cha wiki moja ikiingizwa kificho kutokea mikoa ya jirani.
Mkuu wa wilaya ya mlele Kanali Ngemela Lubinga alisema ng’ombe hao walikamatwa wilayani hapo katika maeneo mawili tofauti ya wilaya hiyo.
Katika tukio la kwanza ng;ombe mia saba walikamatwa katika tarafa ya Inyonga wakitokea mkoani Tabora na tayarai wameisha warudisha huko waliko tolewa.
Kanali Lubinga alieleza ng’ombe wengine 250 wamekamatwa juzi katika mto wa Ugalla walioingizwa kupitia kwenye mto huo kwa kusafirishwa kwa kutumiamitumbwi ya wavuvi.
Alisema wilaya yake ya mlele na mkoa wa katavi imeisha piga marufuku uingizwaji wa mifugo kutokana na kuwa na mifugo mingi kupita kiasi katika mkoa wa katavi
Hali hiyo ya mifugo kuwa mingi ambayo imekuwa ikitoka katika mikoa ya Tabora , Shinyanga, Mwanza, Kigoma na Rukwa imeanza kusababisha uharibifu wa mazingira katika mkoa wa katavi
Amewataka viongozi ambako mifugo hiyo inakotoka waache kutoa vibali kwa wafugaji vya kusafirishia mifugo kwenda mlele na Mpanda kwani uamuzi wa kupiga marufuku mifugo kuingia ndani ya mkoa wa katavi umeishatolewa.
Mkuu huyo wa wilaya ya mlele hivi karibuni alifanya ziara katika tarafa za Inyonga, Nsimbo na Mpimbwe aliwaagiza wananchi wahakikishe hakuna tena mifugo kuingia wilayani hapo.
Na aliwashauri wafugaji katika maeneo hayo wawe na utaratibu wa kupunguza mifugo na wanunue matrekta ambayo yatakuwa yanawasaidia kwa shughuli za kilimo.
0 comments:
Post a Comment