Home » » Taswira Mbalimbali Jinsi Viongozi Wa CCM na Serikali Walivyoung'uruma Katavi

Taswira Mbalimbali Jinsi Viongozi Wa CCM na Serikali Walivyoung'uruma Katavi




Naibu Waziri TAMISEMI,Mh.Aggrey Mwanri akihutubia wananchi wa Mpanda
mkoani Katavi,ambapo aliwasihi kutokubali kudanganywa danganywa na pia
aliwaambia wananchi serikali hii isingependa kuona wananchi wa chini
akionewa, hivyo alitoa tamko la kutowalipisha ushuru wakina mama wafanya
biashara ndogo ndogo mfano vitumbua na chapati.
Naibu Waziri Kilimo na chakula,Mh. Adam  Malima akihutubia wananchi wa
mkoa wa Katavi, juu ya masuala mabali mbali ambayo yametekelezeka
likiwemo suala la umeme na pia aliwaambia wakulima kwamba serikali
imeandaa utaratibu mzuri wa vocha za kilimo ambazo utatangazwa hivi
karibuni.
Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi,Mh. Charles Tizeba akizungumzia masuala
ya kuimarisha reli na pia  utunzaji wa treni zetu ikiwa suala zima la
usafi, pia aliwaambia wananchi serikali imeagiza mabehewa ya abiria na ya
mizigo.
Mh.Nape akihutubia wananchi wa Mpanda waliofurika kwenye  uwanja wa
Kashaulili,ambapo alikemea vikali vitendo vya vyama vingine kuendekeza
vurugu badala ya siasa.
Mh.Mwigulu Mchemba akieleza wananchi masuala muhimu ya kiuchumi na kwa
nini kunakuwa na mfumuko wa bei,pia alitumia fursa hiyo kukemea mauaji
yalotokea kwenye jimbo lake ambapo kijana mmoja kiongozi wa chama
aliuawa na wanachama wa chama cha upinzani
Viongozi wakuu wa Chama cha Mapinduzi wakishiriki maandamano kuelekea kwenye uwanja wa Kashaulili wilaya ya Mpanda.
  Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa-Itikadi na Uenezi, Mh. Nape Nnauye
akisalimiana na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa wilaya ya Mpanda,
mkoa wa Katavi


Chanzo: Haki Ngowi 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa