Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi
Mtu mmoja dreva wa gari aina ya fuso amefariki dunia baada ya kugongwa na roli wakati akiwa ameegesha gari alilo kuwa akiliendesha kwa lengo la kulitengeneza
Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amemtaja aliyekufa kuwa ni Nico Matinya (47) mkazi wa Sumbawanga mkoa wa Rukwa
Ajali hiyo ilitokea julai 11 mwaka huu majira ya saa 2:20 usiku katika mlima wa sijonga tarafa ya Kabungu.
Alisema Nico alikuwa ameharibikiwa na gari alilo kuwa akiliendesha aina ya Fuso lenye namba za usajiri T768 lililokuwa likitokea Tarafa ya karema kuelekea Mpanda mjini
Wakati akiwa anaendelea kutengeneza gari hilo ndipo lilipo tokea gari lenye namba za usajiri T287 AN2 aina ya Fuso lililokuwa likitoka mpanda mjini likielekea tarafa ya karema na lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina moja la Mayeka ambalo lilimgonga na kufa hapo hapo.
Kamanda Kidavashari alisema ajali hiyo ilisababishwa na mwendo kasi wa gari hilo
Dreva wa gari hilo mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo alitokomea kusikojulikana na gari hilo linashikiliwa na polisi wakati wakisubilia mmiliki wa gari hilo ajitokeze kulitambua.
Mwili wa marehemu Nico Matinya umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospital ya wilaya yam panda wakati wakisubiliwa ndugu wa marehemu kuja kuuchukua kutokea sumbawanga kwa ajili ya mazishi
Kamanda Kidavashari ametowa wito kwa madreva kufuata alama za usalama barabarani na kujali usalama wa wamiaji wengine wa barabara.
0 comments:
Post a Comment