Home » » POLISI YASIFU POLISI JAMII KWA KUPUNGUZA UHALIFU KATIKA KATA YA KAKESE MPANDA

POLISI YASIFU POLISI JAMII KWA KUPUNGUZA UHALIFU KATIKA KATA YA KAKESE MPANDA



Na Walter Mguluchuma
Mpanda-Katavi yetu BLOG
Jeshi la polisi  nchini limevutiwa na utaratibu wa ulinzi shirikishi unao fanywa na wananchi wa kata ya kakese wilayani mpanda mkoa wa katavi kwa kufanikiwa kupunguza matukio ya uharifu.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishina wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo Ally Mlege alipo kuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara askari wa jeshi la jadi (sungusungu) pamoja na wananchi wa kata hiyo 

Alisema jeshi la polisi litahakikisha kila afisa wa jeshi hilo anaetoka makao makuu  anapokuwa na ziara katika mkoa wa katavi anafioka kwenye kata hiyo kwa lengo la kujifunza namna ya kata hiyo ilivyofanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya uharifu kwa kutumia ulinzi shirikishi (polisi jamii)

Pia aliwaeleza kuwa wanapowakamata waharifu wahakikishe wanakuwa na vielelezo vya kutosha  ili kupunguza malalamiko kati yao na jeshi la polisi.

Kwa upande wake mtemi wa sungusungu wa kata hiyo ya kakese Martini Ngelenge  alieleza shughuli wanazo zifanya ni kulinda wananchi na malizao na kukamata waharifu.
Alitaja shughuli nyinmgine wanayoifanya ni kuelimisha wananchi waachane na tabia ya uharifu na kujichukulia sheria mkononi kwa kuwachoma moto  waharifu wanaokuwa wamekamatwa 

Nae afisa mtendaji wa kata hiyo Lubeni Kasomo alisema kazoi hiyo ya ulinzi shirikishi katika kata ya kakese pamoja na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa imekuwa ikipambana na changamoto mbalimbali.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pale wanapokuwa wamekamata waharifu wamekuwa wakipata shida ya kuwafikisha katika kituo cha polisi kutokana na kutokuwa na usafiri.

Alitaja tatizo jingine ni zana wanazozitumia kwenye ulinzi ambapo wanatumia silaha za jadi kama vile upinde , mishale na fimbo wakati mwingine huwa  inawauwia vigumu wanapo kuwa wanapambana na waharifu wanao  tumia bunduki.

Aidha kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari aliwahakikishia kuwaondolea tatizo hilo la ukosefu wa usafiri mara wanapo kuwa wamekamata waharifu.
Alisema mara mkamatapo waharifu toweni taarifa polisi na mkiona wamechelewa  kufika nipigieni simu mimi RPC aliwaeleza na huku akiwapa namba zake za simu

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa