Na Walter Mguluchuma, Mpanda, Katavi yetu Blog
Baadhi ya abiria wanaosafiri na mabasi ya kampuni ya sumry katika mikoa ya Katavi na Rukwa wameilalamikia kampuni hiyo kwa kupakia abiria wengi kupita kiasi.
Kero hizo za abilia zilitolewa Julai 19 mwaka huu kwenye kituo cha mabasi cha mpanda mjini wakati wakisafiri kutoka mpanda kwenda Sumbawanga mkoani Rukwa.
Abilia hao walikuwa wakisafiri kwenye basi lenye namba za usajiri T176 BHT ili walazimu kutoa taarifa katika kituo cha polisi baada ya kutoridhika na idadi ya abiria waliokuwa wamepanda kwenye basi hilo.
Mwandishi wa habari hizo alishuhudia mvutano ulio kuwepo hapo baina ya wafanya kazi wa kampuni hiyo pamoja na abilia licha ya askari wa usalama barabarani kufika hapo hawakuweza kuchukua hatua yoyote.
Ndipo alipofika afisa mmoja wa polisi mwenye cheo cha mkaguzi msaidizi Masebo kituoni hapo na kuwaamuru abiria wote waliopanda kwenye basi hilo ambalo wamelipia nauli lakini hawana viti vya kukaa washuke kwenye basi hilo.
Baada ya agizo hilo la afisa wa polisi ndipo abilia wapatao ishirini iliwalazimu kushuka na hatimaye basi hilo liliondoka na kuelekea Sumbawanga.
Mmoja wa abilia aliyeshushwa kwenye basi hilo Eliza Beda alisema kero hizo za abiria kupanda kwenye mabasi ya kampuni hiyo kupita kiasi inasababishwa na kutokuwepo kwa mabasi mengine yanayofanya safari kwenye njia hiyo na kusababisha kampuni hiyo kufanya inavyotaka.
Hivi karibuni Afisa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Katavi Joseph Shilinde alifanya kikao na wamiliki wote wa magari ya abiria ambapo aliwaagiza wafanye shughuli zao kwa kufuata sheria za usalama barabarani
Tatizo la mabasi kubeba abiria mkoa wa Katavi lipo pia katika mabasi yanayo kwenda mkoani Kigoma na Tabora.
0 comments:
Post a Comment