Home » » KAMATI YA USALAMA BARABARANI MKOA WA KATAVI YAJIPANGA KUPUNGUZA AJALI‏

KAMATI YA USALAMA BARABARANI MKOA WA KATAVI YAJIPANGA KUPUNGUZA AJALI‏

Na Walter Mguluchuma wa katavi yetu Blog
Mpanda
Kamati ya usalama barabarani ya mkoa mpya wa katavi  imezinduliwa na imeanza kutafua namna ya kupunguza ajali za barabarani.
Kamati hiyo imezinduliwa ikiwa na wajumbe kumi na tano ambao ni baadhi ya wakuu wa ibadara wanaotoka katika halmashauri ya mji wa mpanda wawakilishi wa vyombo vya usafiri pamoja na askari wa usalama barabarani.
Mwenyekiti wa katati hiyo Nassor Arfi (Tembo mzee) aliitaja mikakati walioipanga  ili kupunguza ajali za barabarani kuwa ni kuwahimiza madreva kwenda kwenye vyuo vinavyotroa mafunzo kama vile Veta ili kuweza kujioingezea uwezo zaidi.
Pia watahakikisha alama za barabarani zinawekwa pamoja na kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara na kuwahimiza madreva kutii na kufuata sheria za usalama barabarani
Mwenyekiti huyo alitaja mkakati mwingine ni kuziondoa gereji bubu zote zilizopo hapa mjini karibu na barabara  ili barabara ziwe wazi
Pia magari yote makubwa yanayoingia mjini hapa kupaki katika maeneo waliyotengewa kama vile ilembe na Misunkumilo.
Kwa upande wake katibu wa kamati hiyo ambaye pia ni afisa usalama barabarani mkoa wa katavi Joseph Shilinde alisema atashughulikia tatizo la magari  kupakia mizigo na abiria kupita kiasi.
Vile vile atawaelimisha wananchi waache tabia waliyoizoea ya kupanda magari ya mizigo (marori).
Shilinde alisema kikosi cha polisi cha usalama barabani kimepanga kuanza kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi  wa shule za msingi  katika mji wa mpanda.
Ajali za barabarani zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku hasa kwa watumiaji wa pikipiki (bodaboda) kutokana na kutofuata sheria za usalama barabarani na eneo jingine mkoani hapa zinakotokea ajari ni kwenye mlima Sijonga  barabara iendayo ziwa Tanganyika katika Tarafa ya Kabungu.
Ambapo gari nyingi zimepata ajari kutokana na kupakia mizigo kupita kiasi na kufanya kushindwa kupanda mlima huo mkubwa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa