Home » » AJALI YA FUSSO YA UWA WA WILI NA MAJELUHI KUMI NATANO WALAZWA HOSPITAL‏

AJALI YA FUSSO YA UWA WA WILI NA MAJELUHI KUMI NATANO WALAZWA HOSPITAL‏

watu wawili wamekufa na wengine Kumi na Tano wamejeruhuwa kufuatia Roli walilokuwa  wakisafiria kupinduka Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea hapo juzi majira ya saa 9:00 Mchana katika Barabara ya Mpanda kwenda Tabora katika eneo la Mlima Kanono.

Aliwataja watu wawili walio kufa kuwa ni:-
Mbungwe Kalemani (34) mkazi wa Mwamkuru Mpanda na 
Kaswendebaza Makude (28) Mkazi wa Salani Mkoani Shinyanga ambaye alikuwa ni utingo wa gari hiyo.

Kidavashari amewataja waliojeruhiwa na kulazwa katika Hospitari ya Wilaya ya Mpanda kuwa ni:-
Gedfrey Jonas (29) Mkazi wa Mwanza aliyepata maumivu ya kifua.
Lucas Charles (30) Mkazi wa Kabage Mpanda 
 Joseph mafulaya (31) Mkazi wa Isege Nzega
Masumbuko Amosi (28) Mkazi wa Sikonge Tabora
Saida Mashauri (32) Mkazi wa Sikonge Tabora
Marco Misayo (30) Mkazi wa NzegaTabora

Wengine ni Ally Shabani (20) Mkazi wa Nzega Tabora, Andrea Deus (25), Ruge Mchele (45), Kizimani Ruge (2) wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.

Kamanda Kidavashari amewataja majeruhi wengine kuwa ni Efulazi Pascal (45) Mkazi wa Inyonga Mlele, Mwazu Makanio(33), mkazi wa Mwamkuru Mpanda na Grece Magembe (22) Mkazi wa Meatu Shinyanga.

Alitaja Gari hilo lililopata ajari ni aina ya Fuso mali ya MAHARAGE Mkazi wa Shinyanga, lenye namba za usajili T476 ARR ambalo lilikuwa likiendeshwa na Dreva aliyetambulika kwa jina moja la EMMANUEL ambaye mara baada ya ajari hiyo alikimbia.

Kidavashari alieleza kuwa Gari hilo lilikuwa limepakia gunia 90 za mpunga kutoka Mpanda kupeleka Kahama.

Chanzo cha ajari hiyo kilisababishwa na Roli hilo kuasha njia na kuelekea polini.

Miili ya marehemu hao wawili bado imehifadhiwa kwenye chumba cha Maiti katika Hospitali ya Mpanda na hari za majeruhi waliolazwa zinaendelea vizuri.

Kamanda Kidavashari ameto wito kwa madreva wa magari kufuata Sheria na kuheshimu Sheria za usalama Barabarani.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa