Mussa Mwangoka, Katavi
POLISI Mkoa wa Katavi imetoa siku 30 kwa wakazi wote wanaomiliki silaha za moto kinyume cha sheria kuzisalimisha kabla ya kuanza kwa msako mkali.
Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Dhahili Kidavashari alisema wananchi watakaosalimisha silaha hizo kwa hiari hawatachukuliwa hatua zozote na msako utaanza baada ya siku hizo kumalizika.
“Baada ya siku hizo 30, polisi wataendesha msako maeneo yote ya mkoa ili kuwabaini wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake” alisema Kidavashari
Alisema watu hao wanapaswa kukabidhi silaha hizo kwenye ofisi zote za serikali zilizopo maneno yao, ofisi za vitongoji, mitaa, vijiji, kata na vituo vya polisi.
Katika hatua nyingine, polisi kwa kushirikiana na askari wa uhamiaji wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 14 na kwamba wamejipanga kudhibiti uhalifu mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment