Home » » AJALI YA LORI YAUA WATATU MKOANI RUKWA NA KATAVI

AJALI YA LORI YAUA WATATU MKOANI RUKWA NA KATAVI


mmoja kati ya majeruhi wa ajali hiyo akiwa wodini

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Rukwa Isuto Mantage amesema ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Fuso lenye namba ya usajiri T620ABA mali ya Eliud Sanga mkazi wa kijiji cha Laela mkoani Rukwa
Mwandishi wa mtandao huu Willy Sumia kutoka Mpanda anaripoti kuwa katika ajali hiyo watu watatu wamefariki dunia na wengine tisa wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya yam panda mkoa wa katavi na wengine katika hospitali ya wilaya ya Nkasi mjini Namanyere
Amewataja waliofariki dunia kuwa ni Maha Lukwetula (51) mkazi wa shankala wilaya ya Mpanda, Kanwa (36) mkazi wa kijiji cha Itenka wilaya ya Mpanda na mtoto wake mwenye umri wa miaka mine (4) ambaye jina lake halikuweza kupatikana
Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Jeshi Charles (33) mkazi wa Namanyere, Juma Lukwetula (40) mkazi wa Shankala, Thomas Simwinga (25) mkazi wa Laela, Sailas Kuzenza (30) mkazi wa Mpalamawe na Linusi Kidomu (36)
Amewataja waliojeruhiwa wengine kuwa ni Shukuru Rafael (9) mkazi wa Laela, Francis Kidomu (24) mkazi wa Londokazi wilaya ya Nkasi na mmoja wao hajafahamika kwani hajitambui hawezi kuongea ambapo wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mpanda
Amesema majeruhi Saidi (25) ambaye amekatika miguu yote miwili amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Nkasi kutokana na hali yake kuwa mbaya
Kamanda Mantage amesema chanzo cha ajali ni kukatika kwa breki za lori hilo lilipokuwa likiteremka mlima Lyamba Lyamfipa Aprili 19, 2012 majira ya saa 8:30 mchana na dereva wa lori hilo anatafutwa na jeshi la polisi baada ya kukimbia mara baada ya ajali kutokea.
MWISHO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa