.jpg)
Na Munir Shemweta, MLELE Waziri
Mkuu Mstaafu ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi
Taifa Mhe. Mizengo Pinda amewataka wanachama CCM wanaotaka kugombea
nafasi yoyote kujiepusha na maneno ya uchochezi yanayoweza kuharibu
mahusiano baina yao. Pinda
amesema hayo tarehe 20 Julai 2024 wakati akizungumza na viongozi
mbalimbali wa CCM wakiwemo madiwani, viongozi wa kata pamoja na wazee
katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi. Amesema,
kwa yoyote anayetaka kugombea nafasi ya uongozi ni vizuri akawa
muangalifu na maneno ya uchochezi aliyoyaeleza kuwa, wakati mwingine
yanaweza kumletea...