Home » » TASAF MKOA WA KATAVI

TASAF MKOA WA KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


 

Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mpango  wa  TASAF   awamu ya   tatu   tangu  ulipoanza   Septemba   2014 Mkoani  Katavi huku  ukiwa   na   kaya  8,537 zilizonufaika  na   mpango  huo na  kwa  sasa   zimebaki    kaya   7,668  kaya   hizo   zimepungua kutokana  na  sababu  mbalimbali  ikiwemo    baadhi ya   wanakaya  kupata  uongozi  katika   Serikali za   Vijiji  na   Mitaa.
  Hayo yalisemwa  hapo  juzi  na    Mratibu wa   Tasaf w a   Mkoa  wa   Katavi   Ignas   Kikwala  wakati wa   mafunzo   ya  wandishi wa   Habari wa   Mkoa wa  Katavi ya   kuwajengea  uelewa kuhusu   mpango  wa  kunusuru  kaya  maskini  yaliofanyika  katika  ukumbi wa   Kichangani     mjini  hapa .
 Alisema     mpango wa  Tasaf   awamu ya   tatu  kwa    Mkoa wa  Katavi  ulianza    rasmi   Septemba 2014 kwa   Halmashauri za   Mpanda,Mlele  na  Manispaa ya  Mpanda  na  kwa   Halmashauri ya   Wilaya ya  Nsimbo ulianza   mwaka   2015  mwezi  septemba .
  Mkoa   huo  una  vijiji  177  ila  vijiji  vinavyotekeleza   mpango wa   Tasaf   awamu ya   tatu  ni     vijiji na mitaa 80 kwa  mwaka huo  2014  Mkoa  ulikuwa  na   kaya  8,537 zilizonufaika  na  mpango  huo  kwa  sasa  zimebaki    kaya  7,668.
  Alisema   kaya  hizo  zimepungua  kutokana  na sababu   mbalimbali  ikiwemo  kuhama kwa   kaya , baadhi ya  wanakaya  kupata   nafasi  za uongozi   katika   Serikali za   Vijiji na   Mitaa,kufariki  kwa wanufaika .
Utekelezaji wa  mpango  toka ulipoanza  mwaka 2014 na   tangu    mpango huo uanza  Mkoani hapa  wameweza  kulipa  kulipa  shilingi  bilioni  6,697,189,679 kwa  kaya 7,668 katika  mizunguko 20 ya  uhawilishaji  fedha .
Kikwala  alieleza  kuwa   Mkoa  pia  umeanza   kufanya   malipo  kwa  wanufaika  273 kwa  njia ya  kielekroniki  kati ya  wanufaika  1,504 waliopo  katika   manispaa ya  Mpanda  na kwa   upande  wa  miradi  ya  ajira   za  muda   jumla ya  walengwa 3,454, wamelipwa  kiasi cha  shilingi ,529,213,900 kwa  Halmashauri ya  Mpanda na   Manispaa ya   Mpanda.
Katika    masuala ya   afya   wanufaika   wa   mpango  wa  Tasaf wamehamasika  na wamejiunga  na  mfuko wa  afya ya jamii  CHF  na  Halmashauri ya   Mlele    ndio inayoongoza  kwa wanufaika wake  1,889 kati ya  2,629 sawa  na   asilimia   72 wamejiunga     na  CHF   na kuongezeka  mahudhurio  kwenye  kiliniki  kwa  watoto   wenye  umri wa kati ya 0    hadi 24.
Kwa  upande  wake   Mwakilishi wa  Mkuu wa  Mkoa wa   Katavi   ambae  pia ni   Mkuu wa    Wilaya ya  Mpanda    Lilian  Matinga    akisoma  hotuba  ya  ufunguzi wa  mafunzo hayo kwa  niaba ya   Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi   aliwataka  Waratibu  wa  Tasaf,    Maafisa  maafisa  wafuatiliaji  wa  Mpango  na  Wandishi wa  Habari kufanya  kazi  kwa ushirikiano  ili  kuhakikisha   wanawaelimisha wananchi juu ya  mpango wa  Tasaf.
 Aliwasisitiza  Waratibu  wa  Mpango  huo  na wahasibu  wa  Halmashauri  kuhakikisha  kuwa  nyaraka   zote  muhimu  za   mpango  ikiwemo    nyaraka  za  malipo  zilizopo   kwenye   Halmashauri   nakala   zake  pia  wahakikishe    zinakuwepo  katika    vijiji na mitaa  iliyokekeleza    mpango huo.
Mwakilishi wa     Mkurugenzi   Mtendaji wa   TASAF     Zuhura     Mdungi  alisema    mpango wa   wa  kuzinusuru  kaya  maskini  unawawezesha   kaya  zilizoandikishwa  kupata ruzuku  ili  kumudu   mahitaji  ya  chakula ,elimu ,afya ,lishe  bora  kwa watoto  na kuwekeza  katika  miradi ya  ujasiriamali .
  Alisema  uujenzi wa miundombinu  ni sehemu ya     mpango wa  kunusuru   kaya  maskini  unalenga  kusogeza  huduma  karibu  na walengwa  na  kuwawezesha  walengwa kutimiza   masharti ya  mpango  na  miradi   inatekelezwa  katika  maeneo  yale tuu yaliofanyiwa  tathimini  na kuonekana  kuwa  yana  upungufu wa huduma za   elimu ,afya  na  maji.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa