Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Kiwango cha ajali za Barabarani na vifo Mkoani Katavi zimepungua kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kutplewa kwa elimu kwa wadau wote wa barabarani na hasa watumiaji wa vyombo vya moto ,na wananchi wengi baada ya kapatiwa elimu ya barabarani .
Hayo yalisemwa hapo jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani Mkoa wa Katavi iliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili Mjini Mpanda ambapo mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alikuwa ni kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Llilian Matinga.
Kamanda Nyanda alisema takwimu za ajari za barabarani kwa mwaka 2016 na 2017 zinaonyesha kwamba ,kwa mwaka 2017 matukio ya ajari yalikuwa ni 55 ukilinganisha na matukio 65 ya ajari yaliotokea kwa mwaka 2016 ambayo ni sawa na upungufu wa matukio 10 ikiwa ni asilimia 15.4.
Alifafanua kuwa Mkoa huo unajumla ya Wilaya tatu na watu waliokufa kwa ajari ni kamaifuatavyo Wilaya ya Mpanda kwa mwaka 2017 walikufa watu 24 wanaume 21 na wanake 3 na mwaka 2016 walikufa watu 20 wanaume 17 na wanawake 3.
Wilaya ya Mlele kwa mwaka 2017 walikufa watu 11,mwaka 2016 walikufa watu 18 na Wilaya ya Tanganyika kwa mwaka 2017 walikufa watu watano ambapo kwa mwaka 2016 walikufa watu 20 hivyo jumla ya watu waliokufa kwa Mkoa mzima wa Katavi kwa mwaka 2017 ni watu 39 wanaume 34 na wanake 5 na mwaka 2016 walikufa 34 wanaume 30 na wanawake wanne.
Alitaja vyanzo vya ajari vilivyosababisha vifo vya watu hao kuwa ni makosa ya kibinadamu yaliyosababishwa na mwendo kasi ,ulevi , na obovu wa vyombo vya moto vya usafiri wa barabarani
Alisema Mkoa huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile watumiaji wa pikipiki BODA BODA kuwanyanyasa wanafunzi kwa vitendo vya ngono na kusababisha mauwaji na alitowa mfano wa tukio la januari 16 mwaka huu lililotokea katika Kijiji cha Vikonge ambapo boda boda alimbaka mwanafunzi na kisha kumuua.
Kaimu Mkuu wa Mkoa Lllian Matinga alisema hari ya matukio ya ajari za barabarani yameweza kupungua kutokana na juhudi kubwa iliyofanywa na jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi ambalo limeweza kufika kwenye vijiji vyote 177 vya Mkoa huu na kutowa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu.
Alisema iliajari ziendelee kupungua na hatimae ziishe kabisa ni vema watumiaji wa vyombo vya usafiri watumie vyombo vyao vya usafiri ambavyo vimekaguliwa .
Aliwataka boda boda kutojihusisha na maswala ya uharifu na askari wa usalama barabarani wanaojihusisha na rushwa waache mara moja kwani kufanya hivyo ni zambi kubwa na wanapaswa kusoma nyakati kwani kwa hari ya sasa kila mtanzania ni TAKUKURU.
Mwenyekiti wa Kamati ya usalama barabarani wa Mkoa wa Katavi Nassor Arfi alisema ajari za barabarani katika Mkoa huo zimeuwa zikisababishwa na sehemu nyingi za barabara kutokuwa na alama za barabarani .
Alisema malengo ya maadhimisho hayo ni kuwapa uelewa wananchi wa kutambua sheria ,kanuni na taratibu za usalama barabarani na jinsi ya kuepukana na ajari za barabarani ambazo hupelekea vifo, majeruhi ,ulemavu na uharibifu wa mali na kupoteza nguvu kazi .
Alisema ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko ambayo yamekuwa yakiwalalamikia baadhi ya askari wa usalama barabarani kuwa wanajihusisha na kupokea rushwa.
0 comments:
Post a Comment