Tuesday, February 13, 2018

MATUKO YA AJALI ZA BARABARANI YAPUNGUA KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Na  Walter  Mguluchuma .
      Katavi .
 Kiwango  cha  ajali  za  Barabarani na  vifo   Mkoani  Katavi      zimepungua kwa  kiasi  kikubwa    hasa   baada ya kutplewa kwa  elimu   kwa   wadau  wote  wa  barabarani     na  hasa  watumiaji  wa  vyombo vya  moto ,na  wananchi wengi   baada ya kapatiwa  elimu ya  barabarani .
  Hayo  yalisemwa  hapo  jana  na  Kamanda wa  Polisi wa  Mkoa  wa  Katavi    Damas   Nyanda  wakati wa  maadhimisho ya   wiki ya  nenda kwa   usalama  barabarani   Mkoa wa  Katavi  iliyofanyika   katika  uwanja wa  Shule ya   Msingi   Kashaulili   Mjini    Mpanda    ambapo  mgeni  rasmi  kwenye  maadhimisho  hayo   alikuwa ni   kaimu   Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi  Llilian   Matinga.
  Kamanda   Nyanda   alisema   takwimu  za   ajari  za   barabarani   kwa  mwaka 2016 na  2017   zinaonyesha   kwamba ,kwa  mwaka   2017  matukio ya  ajari yalikuwa  ni  55 ukilinganisha  na  matukio  65 ya   ajari yaliotokea    kwa  mwaka 2016  ambayo ni  sawa  na  upungufu wa matukio 10 ikiwa ni asilimia  15.4.
 Alifafanua  kuwa  Mkoa  huo unajumla ya  Wilaya  tatu  na watu waliokufa kwa   ajari  ni  kamaifuatavyo   Wilaya ya  Mpanda  kwa  mwaka 2017 walikufa   watu    24 wanaume  21 na wanake  3 na  mwaka  2016 walikufa watu  20 wanaume  17 na  wanawake   3.
  Wilaya ya   Mlele  kwa  mwaka  2017 walikufa watu  11,mwaka 2016 walikufa watu 18 na  Wilaya ya  Tanganyika  kwa  mwaka 2017 walikufa watu watano  ambapo kwa  mwaka   2016 walikufa watu 20 hivyo jumla ya watu waliokufa kwa  Mkoa   mzima wa   Katavi kwa  mwaka 2017 ni watu   39 wanaume  34 na wanake  5 na   mwaka  2016 walikufa  34  wanaume 30 na  wanawake     wanne.
   Alitaja   vyanzo vya   ajari   vilivyosababisha  vifo vya watu hao  kuwa ni  makosa ya  kibinadamu   yaliyosababishwa na  mwendo kasi ,ulevi , na   obovu wa  vyombo vya  moto vya usafiri wa  barabarani
 
  Alisema   Mkoa  huo unakabiliwa  na  changamoto  mbalimbali  kama  vile  watumiaji  wa  pikipiki      BODA BODA  kuwanyanyasa  wanafunzi  kwa  vitendo vya  ngono  na kusababisha  mauwaji na  alitowa  mfano wa  tukio  la  januari  16  mwaka huu lililotokea  katika   Kijiji  cha   Vikonge  ambapo  boda   boda  alimbaka  mwanafunzi  na kisha kumuua.
  Kaimu  Mkuu wa  Mkoa    Lllian   Matinga   alisema  hari ya  matukio ya  ajari za  barabarani    yameweza kupungua  kutokana  na  juhudi  kubwa  iliyofanywa na  jeshi la  Polisi   Mkoa wa  Katavi   ambalo  limeweza kufika  kwenye   vijiji  vyote 177  vya   Mkoa  huu na   kutowa   elimu kwa watumiaji wa   vyombo vya moto na watembea kwa miguu.
  Alisema  iliajari  ziendelee  kupungua  na  hatimae  ziishe  kabisa  ni   vema  watumiaji  wa  vyombo vya    usafiri  watumie  vyombo  vyao  vya usafiri   ambavyo  vimekaguliwa .
  Aliwataka   boda  boda   kutojihusisha  na  maswala  ya  uharifu na   askari wa   usalama  barabarani  wanaojihusisha  na  rushwa waache  mara moja  kwani kufanya  hivyo ni zambi kubwa  na wanapaswa kusoma  nyakati  kwani kwa  hari ya  sasa  kila     mtanzania ni TAKUKURU.
Mwenyekiti wa  Kamati ya  usalama  barabarani wa  Mkoa wa  Katavi  Nassor   Arfi  alisema      ajari za  barabarani   katika   Mkoa  huo   zimeuwa  zikisababishwa  na   sehemu  nyingi za  barabara kutokuwa  na   alama  za  barabarani .
  Alisema  malengo ya  maadhimisho  hayo  ni kuwapa  uelewa  wananchi  wa kutambua   sheria  ,kanuni  na  taratibu  za  usalama  barabarani  na  jinsi ya  kuepukana  na  ajari  za  barabarani   ambazo hupelekea  vifo,  majeruhi ,ulemavu na  uharibifu wa  mali na kupoteza  nguvu kazi .
  Alisema  ofisi yake  imekuwa ikipokea  malalamiko ambayo yamekuwa  yakiwalalamikia  baadhi ya  askari wa  usalama  barabarani  kuwa  wanajihusisha  na kupokea  rushwa.

No comments:

Post a Comment