Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Katavi inamshikilia Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaulolo Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi Kevin Elick Malenge kwa tuhuma za kumkamata akipokea Rushwa ya Tshs 150,000 kutoka kwa mkazi mmoja wa Kijiji hicho ili aweze kumrusu kuishi na kufanya kazi ndani ya Hifadhi ya mstu .
Kaimu Kamanda wa TAKUKURU wa Mkoa wa Katavi Cristophar Nakua aliwaambia jana wandishi wa habari ofisini kwake kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo juzi majira ya saa nne asubuhi katika eneo la Kijiji cha Kaulolo.
Alisema Mthumiwa Kevin alikamatwa kufuatia Takukuru kupatiwa taarifa kutoka kwa msiri wao kuwa Afisa mtendaji huyo ameomba kiasi cha Tshs 200,000 kwa msiri huyo ili aweze kumwingiza ndani ya hifadhi ya mstu ulipo kwenye kijiji hicho ili aweze kuishi huko na kufanya shughuli za kilimo .
Nakua alieleza kuwa baada ya TAKUKURU kupata taarifa hizo ilianza kufanya uchunguzi na kubaini kuwa Afisa Mtendaji huyo amekuwa akijihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea Rushwa kwa watu mbalimbali kwa kupokea kiasi cha kati ya Tshs 150,000 na Tshs 200,000 kwa lengo la kuwaingiza watu kuishi ndani ya hifadhi ya msitu kinyume na sheria .
Baada ya Takukuru kubaini mpango huo wa Afisa mtendaji wa Kijiji kuomba apatiwe Rushwa ya Tshs 200,000 ndipo hapo juzi walipofanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa katika eneo la tukio akipokea rushwa ya Tshs 150,000.
Alisema baada ya mtuhumiwa kukamatwa akipokea fedha alichukuliwa na maafisa wa Takukuru kwa ajiri ya mahojiano zaidi.
Kaimu Kamanda Nakua alisema
mtuhumiwa alikiri kupokea rushwa hiyo na uchunguzi umekamilika sasa
anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa ili kujibu tuhuma zinazomkabii.
Katika hatua nyingine Kaimu Kamanda Nakua
ametoa wito kwa jamii kutojihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea au
kutoa rushwa na haitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaojihusisha
na vitendo vya rushwa hasa viongozi waliopewa thamana na serikali
kulinda rasilimali za Taifa na hifadhi zetu, kwa kufuata kanuni taratibu
na sheria za nchini.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment