Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Uamuzi wa Meya wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Wlliy Mbogo wa kukataa kununuliwa gari la kutembelea umewanufaisha Wananchi baada ya fedha zilizotengwa kiasi cha zaidi ya TSHS Milioni 150 kwa ajiri ya gari lake kutumika kununulia gari la kusombea taka taka .
Awali Manispaa hiyo ilitenga kiasi cha Tshs 159,000,000 kwa ajiri ya gari la Meya ,lakini meya wa Manispaa hiyo Willy Mbogo alikataa na kueleleza fedha hizo zielekezwe kwenye kwenye miradi ya maendeleo kwa kununua gari la kusombea taka .
Gri hilo lori lenye namba za usajiri SM 12244 lenye uwezo wa kubeba tani 16 lilikabidhiwa hapo jana kwa uongozi wa Manispaa hiyo katika ofisi za Manispaa hiyo zilizoko katika Mtaa wa Ilembo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga .
Akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi kwenye makabidhiano hayo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Deodatus Kangu alieleza kuwa Manispaa hiyo ilikuwa imetenga kiasi hicho cha fedha kwa ajiri ya kununulia gari la kutembelea Meya wa Manispaa hiyo ambae hana gari la kutembelea kwa ajiri ya shughuli za manispaa hiyo hata hivyo alikataa kununuliwa gari la badala yake alielekeza fedha hizo zitumike kununua gari la kusombea taka.
Kangu alieleza kuwa fedha hizo ziliizokuwa zimetengwa kutokana na Makusanyo ya mapato ya ndani yaliopatikana katika mwaka wa fedha wa mwaka 2017 na 2018.
Alisema wakazi wa manispaa ya Mpanda huzalisha kiasi cha tani 70.5 za taka ngumu kwa siku sawa na tani 25,732.5 kwa mwaka ambapo asalimia kubwa ya taka hizo ni taka toka majumbani na maeneo ya biashara.
Kaimu Mkurugenzi Kangu alifafanua kuwa kutokana na upatikanaji wa lori lenye uwezo wa kubeba tani 16 litasaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa tatizo la mrundikano wa taka ngumu zilizokuwa zinabaki kwenye viziba au kwenye maeneo yaliyoandaliwa kwa muda mrefu .
Alizitaja baadhi ya changamoto zilizopo katika katika utekelezaji wa udhibiti wa taka ngumu katika Manispaa ya Mpanda kuwa ni upungufu na uchakavu wa malori ya kuzoa taka na kufafirisha taka ngumu .
Changamoto nyingine ni ongezeko la idadi ya wakazi inayopelekea ongezeko la uzalishaji wa taka ngumu na ukosefu wa dampo la kisasa kwa ajiri ya uchambuzi na uzikaji wa taka ngumu .
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lllian Matinga aliitaka Manispaa hiyo kuhakikisha gari hilo linatumika kwa makusudio yake na lisitumike kwa matumizi tofauti na yalivyokusudiwa .
Aliitaka manispaa hiyo kulitunza gari hilo la kulifanyia matengenezo kila yatakapo hitajika na waakikishe gari hilo muda wote linakuwa safi sio kwa kuwa gari hilo ni kakusombea taka basi waliache liwe chafu .
Pia aliishauri Halmashauri hiyo isiishie kununua gari hilo tuu kwani mahitaji ya gari la kusombea taka bado yanahitajika kutokana na jinsi manispaa hiyo inavyokuwa kwa kasi kubwa.
Haidari Sumry Diwani wa Kata ya Makanyagio alimpongeza Meya wa Manispaa hiyo kwa uamuzi wake huo wa kizalendo aliuchukua kwa manufaa ya wakazi wa manispaa na Mkoa kwa ujumla .
Alisema jambo hilo la kubadili matumizi ya fedha zilizokuwa zimetengwa kununulia gari lale ni jambo la kuingwa kwa viongozi wengine.
Nae Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo alisema uamuzi huo aliamua kuutowa sio kwa manufaa yake binafsi bali alitanguliza masilahi ya wananchi kwanza na amewaomba wananchi kuwaunga mkono pindi Manispaa hiyo pindi wanapokuwa wanataka kuongeza kipata cha Halmashauri hiyo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment