Na Walter Mguluchuma
Katavi
Waziri wa Nishati Medadi Kalemani amezita Halmashauri zote hapa Nchini kutenga fedha kwa ajiri ya kuingiza umeme wa Rea kwenye Shule na kwenye majengo yao ya taasisi kwenye maeneo yote ambayo umeme wa Rea umepita .
Wito huo aliutoka hapo jana wakati alipokuwa akiwahutubia Wakazi wa Tarafa ya Inyonga kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Inyonga wakati wa ziara yake ya siku mbili Mkoani Katavi ya kukagua miradi ya mitambo za kufua umeme.
Alisema ni jambo la kushangaza kuona nguzo za umeme zimepita karibu kabisa na shule na kwenye majengo ya taasisi nyingine za Halmashauri huku majengo hayo yakiwa hayana umeme.
Hivyo ni vema kila Halmashauri ikatenga fedha kidogo kwa ajiri ya kuweka umeme kwenye majengo ya taasisi zake kwani gharama ya kuingiza umeme vijijini wa Rea ni Tshs 27,000 tuu hivyo hauni sababu ya Halmashauri kushindwa kulipa fedha hizo kidogo kwa ajiri ya kuingiza umeme kwenye majengo yake .
Kalemani alisema Serikali imepanga na itahakikisha kuwa maeneo yote ya vijiji ambayo hayakufikiwa na umeme wa Rea awamu ya pili vinapatiwa umeme katika mpango wa mradi wa umeme wa Rea awamu ya Tatu.
Alieleza kuwa shirika la umeme Tanzania TANESCO litahakikisha linafunga umeme kwa kaya kwa kaya na mtu kwa mtu bila kujali uzuri wa nyumba au ubaya wa nyumba cha msingi ni mteja awe ametimiza mashariti ya kuingiziwa umeme .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga alisema Mkoa wa Katavi bado unakabiliwa na tatizo la kupata umeme kidogo kutokana na Mkoa huo kutounganishwa na umeme wa Grid ya Taifa hari ambayo inaufanya Mkoa huo kutumia umeme wa Genereta.
Alieleza kuwa Katika Mkoa wa Katavi ipo Wilaya ya Tanganyika ambayo baadhi ya vijiji toka nchi ilipopata uhuru walikuwa hawaja wahi kuona umeme hadi hapo mwaka jana ambapo baadhi ya vijiji vya Wilaya hiyo walipopata umeme wa Rea.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco Alexzanda Kyaruzi aliwaka wananchi kwenye maeneo yaliyofikiwa na umeme wahamasike kutumia umeme kwani kuna maeneo umeme umekuwa ukipotea bure kutokana na baadhi ya maeneo kuwa na watumiaji wachache.
Mwandisi wa Mradi wa kufufua umeme Stephen Manda alieleza Mkoa wa Katavi unategemea mashine tatu za kufua umeme ambapo mbili zipo Mjini Mpanda ambazo zinawezo wa kuzalisha umeme negawati 2.5 na mashine nyingine ipo Inyonga Wilayani Mlele inayozalisha KW 420 ambayo ilianza kufanya kazi mwezi oktoba mwaka jana pia wanategemea umeme wa grid ya Zambia ambao upo kwenye vijiji baadhi vya Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele .
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachal Kassanda alisema pamoja na jenereta ya inyonga kuzalisha KW 420 lakini mpaka sasa matumizi yanayotumika ni KW 71 tuu kwa wateja 335 waliunganishiwa umeme kwa upande wa Halmashauri ya Mlele na kwa wilaya nzima mpaka sasa ni wateja 798 wameunganishiwa .
Aidha jumla ya wateja 336 bado hawajapatiwa umeme bado Serikali ya Wilaya kwa kushirikiana na TANESCO wanaendelea kutowa elimu na kuhamasisha wananchi ili waunganishiwe umeme mapema iwezekanavyo.
mwisho
No comments:
Post a Comment