Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Lilian Matinga ameiagiza Halmashauri ya Nsimbo kuhakikisha inawalipa madeni yote wazabuni wanayoidai Halmashauri hiyo ifikapo Machi 31 na endapo kama watashindwa kuwalipa wazabuni hao ifikapo tarehe hiyo Halmashauri isikope tena kwa wazabuni mpaka hapo wanakapo kuwa wamelipa madeni yao yote .
Mkuu huyo wa Wilaya ya Mpanda alitowa agizo hilo hapo juzi wakati wa kikao cha baraza la biashara la Mkoa wa Katavi TCCIA kilichofanyika katika ukumbi wa idara ya maji mjini hapa .
Matinga alisema Halmashauri ya Nsimbo ndio inayoongoza katika Halmashauri zote tano zilizopo katika Mkoa wa Katavi kwa kuwa na madeni mengi wanayodaiwa na wazabuni mbalimbali ambao wametowa huduma kwenye Halmashauri hiyo kwa kipindi cha muda mrefu sasa.
Alisisitiza kuwa yeye kama Mkuu wa Wilaya amekuwa afurahishwi na tabia ya Halmashauri hiyo kushindwa kuwalipa wazabuni wake na huku bado wakiendelea kukopa madeni mengine kwa wazabuni hao .
Alisema ni jambo la kusikitisha sana kwa Halmashauri kushindwa kulipa hata mzabuni wa chakula hivyo alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo kuhakikisha ifikapo Machi 31 kuhakikisha madeni yote wanayodaiwa na wazabuni wao wawe wameyalipa vinginevyo waache kabisa kukopa kwa wabuni mpaka hapo watakapo kuwa wamelipa madeni hayo alisisitiza DC huyo.
Miongoni mwa wazabuni wanayoidai Halmashauri ya Nsimbo madeni ya toka mwaka 2012 ni wazabuni wa chakula ,stashenali na wakandarasi wa majengo mbalimbali ..
Mwenyekiti wa TCCIA wa Mkoa wa Katavi Hassanal Dalla alisema madai ya wazabuni hao yamekuwa ni ya muda mrefu sasa na yamesababisha baadhi ya wafanya biashara kushindwa kuendeleza shughuli zao .
Alisema wazabuni wamepata usumbufu mkubwa kutoka kwenye taasisi mbaimbali za kibenki ambako wafanyabiashara hao walichukuwa mikopo na wameshindwa kurudisha kwa wakati .
Amani Mahera wa jumuia wa jumuia ya Wafanya biashara Tanzania tawi la Mkoa wa Katavi alieleza kuwa hari hiyo ya kutolipwa kwa wazabuni madai yao kuwewasababishia baadhi yao kufunga biashara zao na wengine kufilisika .
Hivyo aliiomba Halmashauri hiyo kuwalipa fedha zao wazabuni hao ili nao waweze kulipa kodi za serikali kwani inashangaza kwa mfanya biashara kufungiwa kampuni na biashara zake na mamlaka ya kukusanya mapato kwa kosa la kushindwa kulipa kodo wakati nayeye fedha zake zipo anaidai Halmashauri .
MWISHO
No comments:
Post a Comment