Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mpango wa TASAF awamu ya tatu tangu ulipoanza Septemba 2014 Mkoani Katavi huku ukiwa na kaya 8,537 zilizonufaika na mpango huo na kwa sasa zimebaki kaya 7,668 kaya hizo zimepungua kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya wanakaya kupata uongozi katika Serikali za Vijiji na Mitaa.
Hayo yalisemwa hapo juzi na Mratibu wa Tasaf w a Mkoa wa Katavi Ignas Kikwala wakati wa mafunzo ya wandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi ya kuwajengea uelewa kuhusu mpango wa kunusuru kaya maskini yaliofanyika katika ukumbi wa Kichangani mjini hapa .
Alisema mpango wa Tasaf awamu ya tatu kwa Mkoa wa Katavi ulianza rasmi Septemba 2014 kwa Halmashauri za Mpanda,Mlele na Manispaa ya Mpanda na kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ulianza mwaka 2015 mwezi septemba .
Mkoa huo una vijiji 177 ila vijiji vinavyotekeleza mpango wa Tasaf awamu ya tatu ni vijiji na mitaa 80 kwa mwaka huo 2014 Mkoa ulikuwa na kaya 8,537 zilizonufaika na mpango huo kwa sasa zimebaki kaya 7,668.
Alisema kaya hizo zimepungua kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuhama kwa kaya , baadhi ya wanakaya kupata nafasi za uongozi katika Serikali za Vijiji na Mitaa,kufariki kwa wanufaika .
Utekelezaji wa mpango toka ulipoanza mwaka 2014 na tangu mpango huo uanza Mkoani hapa wameweza kulipa kulipa shilingi bilioni 6,697,189,679 kwa kaya 7,668 katika mizunguko 20 ya uhawilishaji fedha .
Kikwala alieleza kuwa Mkoa pia umeanza kufanya malipo kwa wanufaika 273 kwa njia ya kielekroniki kati ya wanufaika 1,504 waliopo katika manispaa ya Mpanda na kwa upande wa miradi ya ajira za muda jumla ya walengwa 3,454, wamelipwa kiasi cha shilingi ,529,213,900 kwa Halmashauri ya Mpanda na Manispaa ya Mpanda.
Katika masuala ya afya wanufaika wa mpango wa Tasaf wamehamasika na wamejiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF na Halmashauri ya Mlele ndio inayoongoza kwa wanufaika wake 1,889 kati ya 2,629 sawa na asilimia 72 wamejiunga na CHF na kuongezeka mahudhurio kwenye kiliniki kwa watoto wenye umri wa kati ya 0 hadi 24.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliwataka Waratibu wa Tasaf, Maafisa maafisa wafuatiliaji wa Mpango na Wandishi wa Habari kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha wanawaelimisha wananchi juu ya mpango wa Tasaf.
Aliwasisitiza Waratibu wa Mpango huo na wahasibu wa Halmashauri kuhakikisha kuwa nyaraka zote muhimu za mpango ikiwemo nyaraka za malipo zilizopo kwenye Halmashauri nakala zake pia wahakikishe zinakuwepo katika vijiji na mitaa iliyokekeleza mpango huo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Zuhura Mdungi alisema mpango wa wa kuzinusuru kaya maskini unawawezesha kaya zilizoandikishwa kupata ruzuku ili kumudu mahitaji ya chakula ,elimu ,afya ,lishe bora kwa watoto na kuwekeza katika miradi ya ujasiriamali .
Alisema uujenzi wa miundombinu ni sehemu ya mpango wa kunusuru kaya maskini unalenga kusogeza huduma karibu na walengwa na kuwawezesha walengwa kutimiza masharti ya mpango na miradi inatekelezwa katika maeneo yale tuu yaliofanyiwa tathimini na kuonekana kuwa yana upungufu wa huduma za elimu ,afya na maji.
No comments:
Post a Comment