Home » » BODABODA WALA KIAPO MBELE YA NAIBU WAZIRI WA AFYA KUWALINDA WASICHANA NA MIMBA ZA UTOTONI.

BODABODA WALA KIAPO MBELE YA NAIBU WAZIRI WA AFYA KUWALINDA WASICHANA NA MIMBA ZA UTOTONI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Na     Walter   Mguluchuma,Nkasi

AGATHA Mwananyau (19) aliyekatiza masomo akiwa Kidato cha Nne  baada ya kupewa ujauzito amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini  ya Sh 300,000/-


Msichana huyo aliyekuwa akisoma Kidato cha Nne  katika Shule ya Sekonadari  Mkangale  katika Mji wa Namanyere  Wilayani Nkasi katika  mkoa wa Rukwa aliacha masomo  baada ya  kupewa ujauzito  na Alfa Nestory (20) .
Mshtakiwa huyo alishindwa  kulipa faini  hiyo ambapo ameanza  kutumikia adhabu  hiyo.


Juzi aliitwa na upande wa mashtaka kutoa ushahidi  katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi  mbele ya Hakimu Ramadhani Rugemalira ambapo alitoa ushahidi wa uongo  akisema kuwa aliyempatia ujauzito  hakuwa mshtakiwa Nestory bali  alikuwa”mmachinga’  aliyetokea Mbeya  tofauti na maelezo yake ya awali .


Ndipo Mwendesha Mashataka , Hamimu Gwelo alipomshtaki kwa kutoa ushahidi wa uongo ambapo jana alifikishwa mahakamani hapo  na aliposomewa mashtaka hayo alikiri  kutenda kosa hilo .


Akitoa hukumu Hakimu Rugemalila alisema kuwa amezingatia  utetezi wa mshtakiwa kuwa apunguziwe adhabu kwa kuwa ana mtoto mchanga mwenye umri wa miezi nane .
Mwisho
Na   Walter   Mguluchuma .   Katavi

ZAIDI ya waendesha pikipiki maarufu “bodaboda” 130 wanaotoa huduma ya usafiri  katika Manispaa  ya Mpanda mkoani Katavi wamekula kiapo cha kuwalinda wasichana  dhidi ya mimba  na ndoa za utotoni .


Kiapo hicho waliapa mbele ya Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo  ya Jamii , Wazee na Watoto , Dk Faustine Ngugulile  jana mjini hapa ambaye alieleza kuwa mkoa wa Katavi  unaongoza  nchini kwa mimba za utotoni kwa  asilimia 45 huku akiutaka uongozi  wa mkoa uone namna ya  kuisadia Serikali  ili wasichana waweze kutimiza ndoto zao.
 


“Hawa waendesha bodaboda  ni ajira kwani wapo baadhi yao wamejenga nyumba na kusomesha watoto  wao  kamwe wasionekane kama wahuni  isopkuwa jamii iwape ushirikiano “ alisisitiza .


Bodaboda hao waliahidi mbele ya Naibu Waziri kuwa  kwa kuwa  pikipiki zao  vimekuwa  vikitumika  kuwapeleka  wasichana  wengi wao wakiwa ni wanafunzi  kwenye  nyumba za kulala  wageni.


Hivyo watahakikisha kuanzia sasa watakuwa wanatoa taarifa kwa wazazi , walezi  na Jeshi la Polisi  pindi watakapom baini   msichana waliyembeba na kumpeleka  kwenye nyumba ya kulala wageni akiwa na umri  mdogo .


  Walisema wao  binafsi  watajizuia  kufanya  vitendo  vya ukatili  wa kingono dhidi  ya  watoto  katika   sehemu  yoyote  ile watakapo kuwepo  kwamba wapo baadhi yao wamechangia  mimba za utotoni kwa kuwashawishi wasichana kufanya nao ngono .


Walieleza kuwa  ni  aibu  mkoa wao (Katavi) kuwa ni kinara wa mimba za utotoni nchini  wakiahidi kuwa  watahakikisha  wanalipunguza tatizo hilo  mkoani humo .
.Nae Mwenyekiti wa  waendesha “Bodaboda”, Stephano Asalile alisema kabla ya kula kiapo hicho walipewa  mafunzo na maofisa  mkoa Wa  Katavi  waliotoka  Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia ,Wazee na Watoto jinsi ya kuwalinda watoto na kuzuia mimba za utotoni .


“Matunda ya mafunzo hayo yameanza kuonekana kwani tayari tumesha toa  tarifa Jeshi la Polisi  ambapo wanaume kumi wameshakamatwa wakituhumiwa kufanya ngono  na wasichana wenye umri mdogo “ alieleza




 Mwendesha ‘bodaboda “ , Leonard Wilson  wazazi wakashirikiana na wao kwani kumekuwepo  na tabia  ya wasichana wadogo  kujiuza  katika nyumba za starehe .
Mwisho

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa