Home » » WATU WAWILI WAWILI WAKAMATWA NA TAKUKURU WAKIPOKEA RUSHWA NJE YA JENGO LA IKULU NDOGO BAADA YA KUJIFANYA KUWA WAO NI MAAFISA WA TAKUKURU WA MKOA WA KATAVI

WATU WAWILI WAWILI WAKAMATWA NA TAKUKURU WAKIPOKEA RUSHWA NJE YA JENGO LA IKULU NDOGO BAADA YA KUJIFANYA KUWA WAO NI MAAFISA WA TAKUKURU WA MKOA WA KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399

Na  Walter  Mguluchuma.
         Katavi .
  Taasisi ya  kupambana na kuzuia  Rushwa  TAKUKURU  Mkoani  Katavi  imewakamata   Nicodemo  Peter  na      Peter   Mwaninsawa   wakazi wa  Mtaa wa  Nsemlwa   Manispaa ya  Mpanda  kwa  tuhuma za kupokea  Rushwa   Wakati wakiwa   nje ya  jengo la Ikulu ndogo ya  Mkoa wa  Katavi ya  Tshs  400,000 baada ya  kuijifanya wao ni maafisa wa TAKUKURU .
 Wahumiwa  hao wawili walikamatwa  hapo  jana   majira ya saa  nne   asubuhi wakiwa  wanapokea   kiasi  hicho  cha  fedha katika  eneo    la  nje  ya  jengo    la  Ikulu  ndogo ya  Mkoa wa  Katavi  iliyopo  jirani na    ofisi ya  TAKUKURU.
Kamanda wa  Takukuru wa  Mkoa wa   Katavi  John   Minyenya  aliwaambia  wandishi wa   Habari  jana  ofisini  kwake  kuwa watuhumiwa  hao walikamatwa  kufuatia   mtego  uliondaliwa  na  taasisi  hiyo  baada ya kuwa wamepata taarifa kutoka kwa msiri wao juu ya watu hao waliokuwa wakijiita ni  maafisa wa  TAKUKURU  wa  kitengo cha  uchunguzi .
 Alisema  kabla ya  kukamatwa kwa wahumiwa  hao walimpigia  simu    msiri wa  TAKUKURU  na  kujitambulisha  kuwa  wao ni   maafisa wa   TAKUKURU   na wanalo  jalada la uchunguzi za  huhuma   zinazo  mkabili    msiri  huyo .
  Hivyo walimtaka   awape  kiasi cha   shilingi    laki   nne  ili  waweze  kulifunga   jalada kwa  kufuta  tuhuma zilizomkabili  msiri   huyo  ambae   ni   Mtendaji wa  Kijiji  cha  Vikonge  Wilayani   Tanganyika   ambae walidai  kuwa   alikuwa na  tuhuma za   kupokea  rushwa ya kutoka  kwa wafugaji  ambao   alikamata  mifugo ya  wafugaji na kisha   aliiachia  baada ya kupokea   Rushwa kiasi cha  Tshs  2,500,000 .
  Minyenya  alieleza kwa  kuwa   msiri  huyo    ambae   hapendi   na  anapinga   Rushwa  alilazimika  kufika  kwenye   ofisi ya  Takukuru  na  kutowa  taarifa juu ya  maafisa  hao   bandia wa  Takukuru .
Ndipo   Takukuru walipoanza  kufanya  uchunguzi juu ya  malalamiko  hayo     kutokana  na  TAKUKURU  kutokuwa  na  watu  wenye  tabia  kama  hiyo ya  kuomba  na  kupokea  Rushwa .
Alisema  ndipo  hapo  TAKUKURU  walipoandaa  mtego wa kuwakamata  watuhumiwa  hao  ambao walimtaka  msiri  huyo   awapelekee  fedha  hizo   nje ya   jengo la   Ikulu  ndogo ya  Katavi kwa  kuwa  ni  jirani na  ofisi  yao ya  Takukuru  ili   iwe  rahisi wao kutoka   ndani ya   osisi  ya  TAKUKURU  Na  na kufika  kwenye   eneo la  tukio.
Kufuatia  makubaliano  hayo   msiri ulipofika   muda wa  kupeleka    fedha  kwa  maafisa  hao   bandia  alikwenda  kuchukua  fedha   zilizokuwa  na   namba  za  TAKUKURU  na  kisha   aliwapelekea   kwenye   eneo  walilokuwa  wamekubaliana kwa  ajiri ya   kubabidhiana  na  mara tuu walipo  pokea   fedha  hizo  nje ya   njengo la  Ikulu watuhumiwa  hao  walikamatwa  na  Maafisa wa  TAKUKURU  huku wakiwa na  fedha  hizo .
Kamanda   Minyenya  alisema  watuhiwa  hao  wanaendelea kushikiliwa  na  watafikishwa  mahakamani  ili   wakaweze  kujibu  mashita  mawili  ambayo ni  kujifanya  maafisa wa  Takukuru  na  shitaka la  pili ni  kuomba na  kupoke  rushwa .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa