Home » » DIWANI JELA MIAKA MITATU KWAKOSA LA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA YA TSHS 500,000.

DIWANI JELA MIAKA MITATU KWAKOSA LA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA YA TSHS 500,000.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter   Mguluchuma,    Katavi
DIWANI  wa Kata ya Katumba (CCM) , Seneta Jeris  Baraka (32)  amehukumiwa  na Mahakama ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi  kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kutiwa hatiani  kwa makosa mawilli ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh500,000/-


Akisoma hukumu hiyo jana  , hakimu wa mahakama hiyo , Tetimus Swai alisema kuwa mshtakiwa  alitiwa hatiani kwa makosa mawili  ya kuomba rushwa  ya Sh 1,000,000/- na kupokea rushwa  ya Sh 500,000/- kutoka kwa mfugaji aitwae  Charles Kiligiwa maarufu kama Mange .

Akimuhukumu alisema mshtakiwa huyo katika kosa lake la kwanza atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela  au kulipa faini ya Sh 500,000/- na katika kosa la pili atatumikia kifugo cha miaka mitatu bila faini .

“Hivyo mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela bila kulipa faini na haki yake  ya kukata rufaa iko wazi “ alihukumu Swai .

Awali Mwendesha Mashtaka wa Tassisi ya Kupambana na Kuzuai Rukwa (Takukuru) ,  Bahati  Haule alidai mahakamani hapo kuwa Desemba 20,2017  Mahakama ya Mwanzo  katika Kambi  ya Wakimbizi wa Burundi  ya Katumba  iliamuamuru mfugaji Kiligiwa maarufu Mange  atoe mifugo yake ytote aliyoiingiza kambini humo kinyume cha sheria  kabla ya  Desemba 21 , 2017 .

Aliongeza kuwa  ndipo  mshtakiwa alimshawishi mfugaji huyo  ampatie kiasi cha Sh 1,000,000/-  ili asitekeleze amri  hiyo iliyotolewa na makakama hiyo  kwamba asiitoe mifugo yake kambini humo .

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka Haule mfugaji huyo alimpatia mshtakiwa huyo  kiasi cha Sh 100,000/- ikiwa ni malipo ya awali .

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Mei , 11, mwaka jana  mshtakiwa alimtaka mfugaji amlipe kiasi kilichobakia  ,ndipo  mtego  ulitengwa  katika maofisa wa Takukuru  na mfugaji ambapo alimtaka mshtakiwa wakutane katika kijiji cha Ivyungwe  amlipe kiasi cha Sh 400,000/ ili nusu iliyobakia amlipe siku za usoni .

Katika utetezi wake mshtakiwa aliiomba mahakma impunguzie adhabu kwa kuwa ana familia  na mama mazazi ambaye ni mzee sana wote wakimtegemea kwamba   ni mara yake ya kwanza  kushtakiwa mahakamani .
Mwisho





0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa