NA Walter Mguluchuma .
Katavi .
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda katika Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa Halmashauri 18 za hapa Nchini iliyo katika mpango wa uborereshwaji wa miundo mbinu ya Miji yaani ULGSP uliopangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano na jumla ya miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni Tshs 11 750,000,000 imepangwa kutekelezwa katika Manispaa ya Mpanda .
Hayo yalielezwa hapo jana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Enelia Lutungulu wakati wa mkutano wa wadau wa mpango kabambe wa Master plan ya miaka 20 ya Manispaa hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Mpanda .
Alisema mpango wa uboreshaji wa miundo mbinu katika Halmashauri hiyo ulianza toka mwaka wa fedha wa 2013 na 2014 na utakamilika katika mwaka wa fedha wa 2017 na 2018.
Kwamujibu wa sense ya watu ya mwaka 2012 Manispaa hiyo ilikuwa na jumla ya wakazi 102,900 hivyo kupelekea kwenye mpango huo kupata mgao wa Dola USD 7,342,975, kwa muda wa kipindi cha miaka mitano ambazo ni sawa na Tshs Bilioni 11,750,000,000.
Lutungulu aliitaja miradi saba iliyopangwa kutekelezwa kwenye mradi huo kuwa ni usanifu wa miradi ya msoko, barabara na ujenzi wa soko la kisasa katika Kata ya Kazima, ujenzi wa Stendi ya mabasi ya kisasa katika eneo la Ilembo, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha rami za kilometa 7.7 Mpanda Mjini na uandaaji wa mpango kabambe wa Manispaa ya Mpnda na kujenga uwezo .
Mradi huo utakekelezw na mtaalamu mshauri City Plan Consultancy T Limeted kwa gharama ya Tshs 283 600,000 Fedha ambazo zimetolewa na Manispaa ya Mpanda kupitia mpango wa utekelezaji wa Miji unaofdhiliwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia .
Alifafanua kuwa mpango kabambe wa Master Plan wa Manispaa hiyo ulitangazwa kuanza mwaka 2010 lakini ulisimamishwa kutokana na kuongezeka kwa maeneo ya utawala hivyo mpango huu unatangazwa upya .
Iddy Mwerangi Afisa Mipango miji mshauri wa City Plan Consultancy T Limeted alisema kuwa ni lazima nguvu ziunganishwe za wadau mbalimbali wanaoweza kusaidia kupatikana kwa taarifa mbalimbali zitakazowezesha uaandaaji wa mpango Kabambe .
Alisisitiza kuwa swala hilo linahitaji sana kushirikisha wananchi kwani uzoefu unaonyesha kuwa maeneo ambayo wananchi wamekuwa hawashirikishwi kumekuwa na migogoro .
Makamu wa Meya wa Manispaa ya Mpanda John Matongo alisema swala hilo bila ushirikiano wa wananchi haliwezi kufanikiwa hivyo wao kama madiwani watahakikisha zoezi hilo la mpango Kabambe wa Master Plan linafanikiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga alisema kuwa Mji wa Mpanda unakuwa kwa kasi sana hivyo ni vema maeneo ya mji huo yakawa yamewekwa kwenye mpango unaoeleka .
Alisema kuwa katika mpango huo waakikishe pia wanatenga maeneo kwa ajiri ya wakulima na wafugaji kwani kwa sasa yapo baadhi ya maeneo watu wanashindwa kulima kutokana na wafugaji kuvamia maeneo ya wakulima .
Nchi hii inaendeshwa kwa misingi ya sheria na hakuna mtu aliyejuu ya sheria hivyo kwa mtu yoyote ambae ataamua kuishi kinyume na utaratibu wa matumizi bora ya ardhi yalivyo pangwa ajuwe kuwa hatua lazima zitachukuliwa dhidi yake alisema mkuu huyo wa Mkoa .
0 comments:
Post a Comment