Friday, October 6, 2017

MANISPAA YA MPANDA KUTUMIA ZAIDI BILIONI 11.75 KWA AJILI YA UBORESHWAJI WA MIUONDO MBINU.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

NA  Walter  Mguluchuma .
       Katavi .
 Halmashauri ya  Manispaa ya  Mpanda   katika  Mkoa wa Katavi  ni miongoni mwa  Halmashauri 18 za  hapa  Nchini iliyo katika   mpango  wa  uborereshwaji  wa miundo mbinu  ya Miji  yaani ULGSP  uliopangwa  kutekelezwa  kwa kipindi cha miaka mitano  na jumla ya miradi saba  yenye thamani ya  shilingi  bilioni   Tshs  11 750,000,000  imepangwa  kutekelezwa katika Manispaa ya Mpanda .
  Hayo  yalielezwa  hapo jana  na  Kaimu    Mkurugenzi wa   Halmashauri ya  Manispaa ya   Mpanda     Enelia   Lutungulu  wakati wa    mkutano  wa  wadau  wa  mpango   kabambe  wa   Master   plan ya miaka 20 ya  Manispaa  hiyo uliofanyika  katika   Ukumbi wa  Manispaa ya  Mpanda .
Alisema   mpango wa  uboreshaji wa   miundo  mbinu katika  Halmashauri hiyo  ulianza  toka  mwaka  wa fedha wa  2013 na 2014 na  utakamilika katika  mwaka wa fedha wa  2017 na 2018.
Kwamujibu wa   sense  ya watu   ya  mwaka 2012  Manispaa  hiyo ilikuwa na jumla ya wakazi  102,900 hivyo kupelekea kwenye   mpango huo kupata  mgao wa  Dola   USD   7,342,975, kwa  muda wa kipindi cha miaka mitano  ambazo ni sawa na  Tshs  Bilioni   11,750,000,000.
Lutungulu  aliitaja  miradi saba  iliyopangwa kutekelezwa  kwenye  mradi huo kuwa ni   usanifu wa miradi ya msoko, barabara  na ujenzi wa  soko la kisasa  katika   Kata ya Kazima, ujenzi wa  Stendi ya  mabasi ya  kisasa   katika  eneo la  Ilembo, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha  rami  za kilometa 7.7  Mpanda   Mjini  na   uandaaji wa   mpango    kabambe  wa  Manispaa ya  Mpnda  na   kujenga uwezo .
Mradi  huo   utakekelezw  na   mtaalamu  mshauri    City   Plan   Consultancy     T  Limeted kwa  gharama ya   Tshs   283 600,000   Fedha  ambazo  zimetolewa na   Manispaa ya  Mpanda  kupitia   mpango wa  utekelezaji  wa  Miji   unaofdhiliwa  kwa   mkopo wa  Benki ya   Dunia .
 Alifafanua kuwa     mpango  kabambe wa   Master  Plan wa   Manispaa hiyo ulitangazwa kuanza mwaka   2010  lakini  ulisimamishwa  kutokana  na kuongezeka kwa  maeneo ya  utawala   hivyo  mpango huu  unatangazwa  upya .
Iddy    Mwerangi     Afisa    Mipango      miji    mshauri  wa  City   Plan    Consultancy   T    Limeted  alisema    kuwa ni  lazima  nguvu   ziunganishwe  za  wadau  mbalimbali  wanaoweza  kusaidia  kupatikana  kwa  taarifa   mbalimbali   zitakazowezesha  uaandaaji  wa   mpango    Kabambe .
Alisisitiza  kuwa   swala  hilo   linahitaji  sana   kushirikisha   wananchi  kwani   uzoefu   unaonyesha  kuwa   maeneo   ambayo wananchi wamekuwa   hawashirikishwi kumekuwa na migogoro .
Makamu wa  Meya  wa  Manispaa ya  Mpanda   John   Matongo   alisema   swala  hilo    bila   ushirikiano wa   wananchi   haliwezi kufanikiwa  hivyo  wao  kama   madiwani  watahakikisha   zoezi   hilo la   mpango   Kabambe wa  Master   Plan  linafanikiwa.
Mkuu  wa  Mkoa  wa   Katavi   Meja    Generali   Mstaafu    Raphael   Muhuga   alisema  kuwa   Mji wa  Mpanda   unakuwa  kwa   kasi   sana   hivyo    ni    vema   maeneo ya   mji huo  yakawa   yamewekwa  kwenye    mpango    unaoeleka  .
  Alisema  kuwa  katika   mpango huo  waakikishe  pia   wanatenga   maeneo   kwa   ajiri ya   wakulima  na  wafugaji    kwani kwa  sasa  yapo  baadhi ya  maeneo   watu  wanashindwa kulima   kutokana  na  wafugaji kuvamia  maeneo ya wakulima .
Nchi  hii   inaendeshwa  kwa   misingi ya   sheria  na  hakuna   mtu    aliyejuu ya    sheria   hivyo  kwa  mtu  yoyote   ambae   ataamua  kuishi     kinyume  na   utaratibu wa  matumizi bora ya  ardhi yalivyo   pangwa    ajuwe kuwa  hatua   lazima   zitachukuliwa  dhidi yake   alisema   mkuu  huyo wa   Mkoa .

No comments:

Post a Comment