Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi kimefanya uchaguzi wa ngazi ya Wilaya na kuwapata viongozi wa Chama hicho watakao kwa kipindi cha miaka mitano ijayo huku Walfugang Mizengo Pinda ambae ni mdogo wake na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo .
Uchaguzi huo ulifanyika juzi katika ukumbi wa Chama cha Msingi Ukonongo ulipo Inyonga Wilayani Mlele na mgeni rasmi kwenye Mkutano huo alikuwa ni Waziri mteule wa Wzira ya Maji Eng Izack Kamwelwe ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Katavi .
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano huo wa Uchaguzi msimamizi huyo wa uchaguzi aliwaasa wajumbe wa mkutano huo kujiepusha na kuwachagua viongozi watakao washawishi wawachangue kwa ajiri ya kuwapatia rushwa .
Akitangaza matokea hayo ya uchaguzi msimamizi wa uchaguzi huo Katibu Mwenezi wa CCM wa Mkoa wa Katavi Joseph Makumbule alisema idadi ya wajumbe waliotakiwa kupiga kura 541 ambao walikuwa wametoka kwenye Kata 15 za Wilaya hiyo lakinii waliohudhuria ni wajumbe 477.
Makumbule alifafanua kuwa wagombea walikuwa ni watatu kwenye nafasi ya Mwenyekiti ambapo kura zilizopigwa zilikuwa ni 477 ambapo kura moja iliharibika na matokeo yalikuwa ni Gerald Kasela alipata kura 146 John Mbogo kura 110 na Walfffugang Mizengo Pinda kura 220.
Kwa mujibu wa Kanuni mshindi wa nafasi hiyo lazima avuke nusu ya kura hivyo wajumbe wa mkutano huo walilazimile wapige kura kwa mara ya pili kwa wagombea wawili walipata kura za juu ambao ni Gerald Kasela na Walfugang Mizengo Pinda .
Ambapo katika uchaguzi huo wa marudio kura 450 zilipigwa ambapo Gerald Kasela alipata kura 156 na Walfugang Mizengo Pinda alipata kura 280 na kura 8 ziliharibika hivyo msimamizi wa uchaguzi Joseph Makumbule alimtangaza Walfugang Mizengo Pinda kuwa ndio mshindi w nafasi hiyo na alimtangaza rasmi kuwa Mwenyekiti wa Wilaya wa CCM wa Wilaya ya Mlele.
Pia mkutano huo ulimchagua Renatus Kamaninja kuwa Katibu Mwenezi wa Wilaya baada ya kuwashinda wagombea wenzake watatu na Lachael Kasanda ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele alichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa baada ya kuwashinda wagombea tisa wa nafasi hiyo .
Na kwa upande wa Wilaya ya Mpanda Abal Hamis Kimanzi alchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Wilaya hiyo baada ya kuwashinda Method Mtepa na Wense Kaputa waliogombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi uliofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Azimio Mjini hapa.
Nafasi ya Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Mpanda alichaguliwa Elias Milwano ambae aliwashinda wagombea wawili waliokuwa wameomba nafasi hiyo .
0 comments:
Post a Comment