Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mamlaka ya usimamizi wa Wanyama pori Tanzania TAWA inatambua kuwa mafanikio ya uhifadhi hapa Nchini hayawezi kupatikana bila kuwepo utulivu kwenye maeneo ya hifadhi kutona na ujangili ,uvamizi wa maeneo ya uhifadhi hivyo TAWA itaendelea kuimarisha uwezo wa ndani katika kupambana na ujangili na kudhibiti uvamizi wa mifugo na kilimo kwenye maeneo ya mapori ya akiba na tengufu.
Kauli hiyo ilitolewa hapo jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Dkt James Mwakibara wakati wa kufunga mafunzo ya jeshi usu kwa Maafisa 59 wa kutoka TAWA yaliokuwa yakifanyika kwenye kituo cha mafunzo cha Mlele Mkoani Katavi .
Alieleza lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwaandaa watumishi wa TAWA kufanya kazi katika mfumo wa kijeshi PARAMILITARY ili kuboresha utendaji kazi kwa kujifunza mbinu za kupambana na ujangili ,kuimarisha nidhamu ya watumishi na kuboresha mtiririko wa kutoa na kupokea amri.
Alisema katika swala nzima la kuapambana na ujangili hapa nchini TAWA inaendelea kushirikiana na Taasisi za uhifadhi na vyombo vya dola pamoja na wananchi katika kupambana na ujangili.
Alieleza kuwa wanaelewa jitihada zinazofanywa na Bodi ya Mamlaka hiyo za kuhakikisha wanapata zana za kufanyia kazi ikiwemo kupata sheria ya Mamlaka na Strategic plan itakayo saidia kuwapa nguvu katika kutekeleza kazi zao.
Dkt Mwakibara alisema TAWA ni Shirika kubwa na limetapakaa Nchi nzima inamiliki maeneo ya wanyama pori makubwa mara mbili zaidi ya TANAPA na mara 13 zaidi Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro NCAA.
Ukubwa wa eneo hilo ni mtaji katika uchumi na uzalishaji ili kufikia malengo yaliowekwa wanapaswa kuwa wabunifu kwenye kuongeza mapato na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya Nchi .
Alifafanua kuwa katika mwaka wa fedha wa 2016 na 207 Mamlaka ilipanga kukusanya jumala ya shilingi Bilioni 40 lakini zilikusanywa shilingi Bilioni 36 kwa hiyo ni jukumu lao wote kuhakikisha wanapandisha mapato ili kuweza kutimiza malengo na kuweza kutatua changamoto za uhaba wa vitendea kazi na kuboresha miundo mbinu.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania TAWA Meja Generali Mstaafu Hamis Semfuko alieleza kuwa ni mategemeo yake kuwa mafunzo walipatiwa maafisa hao wa Kati wa TAWA yatawaongezea nguvu katika kupambana na ujangili na changamoto nyingine ikiwemo matumizi ya silaha za kivita katika ujangili na uvamizi wa maeneo ya hifadhi.
Alisema katika kuboresha ulinzi wa rasilimali za nchi katika maeneo yaliochini Bodi ya Tawa ilisha towa agizo kwa Manejimenti kuhakikisha kwamba Ofisi zote za wakuu wa vituo zinahamia kwenye maeneo ya mapori husika badala ya kuwa mijini .
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa ambae ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi Izumbe Msindai aliwaka watumishi wanofanya kazi kwenye Hifadhi na mapori ya akiba pamoja na tengefu waepuke kujihusisha na maswala ya Rushwa kwani wapo baadhi mwa wtumishi wamekuwa sio waaminifu .
Mkufunzi Mkuu wa mafunzo hayo Mhifadhi Fidelis Kapalata alisema wahitimu hao wamepatiwa mafunzo hayo kwa muda wa wiki sita na yamewajengea utimamu wa mwili na mbinu za kupambana ujangiri pia ujasiri wa kujiamini na hari katika kulinda rasilimaii za wanyama .
0 comments:
Post a Comment