Home » » WAKULIMA WA TUMBAKU WALALAMIKIA TUMBAKU YAO KUTONUNULIWA NA KUTOLIPWA PESA ZAO.

WAKULIMA WA TUMBAKU WALALAMIKIA TUMBAKU YAO KUTONUNULIWA NA KUTOLIPWA PESA ZAO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

           Na   Walter  Mguluchuma .
                       Katavi .
Wakulima wa   Chama  cha  Msingi  cha wakulima wa   Tumbaku  cha  Mpanda    Kati  kilichoko   katika  Mkoa wa  Katavi  wameilalamikia  Bodi ya  Chama  hicho  kwa kuwaruhusu  walanguzi wa  Tumbaku  wanaonunua  Tumbaku   ya  kutoka   Mkoa wa  Tabora na  kuwaruhusu walanguzi hao kuuza  Tumbaku  mfululizo  katika  masoko  na kuwakwamisha wanachama  wa  chama hicho kuuza  Tumbaku yao waliozalisha.
  Malalamiko  hayo ya   Wanachama wa  Chama  hicho  cha  Msingi      cha  ushirika wa  wakulima wa  Tumbaku  yalitolewa  hapo  jana  na  wakulima   hao   mbele ya  wandishi wa  Habari  katika  ofisi za   Chama  hicho  zilizopo  katika    Mtaa wa   Madukani   Mjini  hapa .
  Ramadhan  Nassoro     mmoja  wa    wakulima  hao  alisema    wakulima  wa  chama  hicho  wameshindwa kuuza  Tumbaku  yao ya   zaidi ya  kilo   laki  tano  ya    msimu  wa  ununuzi wa  Tumbaku wa  mwaka  2016 na  2017  kutokana  na   sababu  mbalimbali .
  Alizitaja   sababu  hizo kuwa   zimesababishwa  na   kitendo  cha   bodi ya   chama   hicho kuwaruhusu  walanguzi wa   Tumbaku  kuuza   tumbaku yao ya  kutoka  Mkoa wa   Tabora  na   Mishamo   Wilaya ya   Tanganyika   kwenye  masoko ya  chama  hicho  hari  ambayo  imesababisha  wakulima wa    chama  hicho  kushindwa  kuuza  tumbaku  kwenye   chama  hicho kufuatia   idadi ya  kilo walzokuwa wamekubaliana  na  Kampuni  inayonunua  Tumbaku  ya  PREMIUM   kukamilika .
Nae   Sef  Bakari   alieleza  kuwa  yeye ni  miongoni mwa  wakulima   waliouza  tumbaku yao  kwenye  chama   hicho  lakini   mpaka  sasa malipo  yake   bado  haja  lipwa  kwa  kile  kinachodaiwa  kuwa hawezi  kulipwa  malipo yao  mpaka  hapo   kampuni ya  PPEMIUM  itakapo  kubali  kununua  zaidi ya kilo  laki tano  zilizozidi.
  Alifafanua  kuwa  swala  la  kuzidi kwa  kilo  za  Tumbaku    wao  wakulima  haliwahusu  bali   wao wanachohitaji  ni  kulipwa  kwa  fedha  zao tuu kwani tatizo  hilo  limesababishwa na  viongozi wa  chama  hicho  kushirikiana  na  walanguzi  kwa kuwaruhusu kuuza  tumbaku ya kutoka nje ya  chama  chao .
 Aliomba  Serikali ya  Mkoa   iunde tume ya  kuchunguza kwa  nini  kilo  za  tumbaku  zimezidi kwa  kiasi    hicho  kitu  ambacho  hakija  wahi kutokea  katika  miaka ya  uko  nyuma na  alishauri  kwenye   tume  hiyo na  wakulima  washirikishwe.

  Richard  Selevesto   alieleza  kuwa  wamekuwa  wakijiuliza  bila  kupata  majibu  kwani   inakuaje  watu  wale  wale  wa siku  zote  kila mwaka  wao tuu  ndio  wanaongoza kwa  kuuza  tumbaku  kila   soko  na  mtu  mmoja  anauza  tumbaku   mpaka   mitumba  600 wakati aliilingani  na  kilimo  chao  na  viongozi wanawaangalia tuu na  swali la  kujiuliza  mashamba  yao  yako  wapi  waliyovuna   hizo tumbaku  zote .
Noelia   Mbambali   aldai  kuwa  yeye  tumbaku yake  inazaidi ya   mwezi  mmoja   sasa  na   ipo  ndani ya   ghara la  chama  hicho  lakini  imeshindwa  kununuliwa  hadi  sasa kwa  kisingizio  cha   kutimia  kwa  idadi ya  kilo  zinazotakiwa  kununuliwa  na  kampuni.
Nae    Osca   Paulo     alisema  kuwa   wanaimani  kuwa   bila  walanguzi  kuingiza  tumbaku  yao  kwenye  masoko  yangekuwa  yameisha   malizika   na  hata  malipo  wangekuwa wamelipwa  wakulima   ndio  maana  tunasema       walanguzi na   viongozi   wetu  wanawahujumu  wakulima  wanyonge .
Makamu  Mwenyekiti wa   chama  hicho   Moses   Shila    alieleza  kuwa   chama   chao  kiliwekeana  na   Kampuni  ya   ununuzi ya   tumbaku  ya   Premium kununua  kilo   1,400,000  kwa  msimu  huu  na   tayari   zimeisha   timia   hivyo   mazungumzo     yanaendelea na   kampuni  hiyo  ili   iweze  kununua  kilo   zaidi ya   laki   tano  zilizo  zidi .
  Alisema     endapo   kampuni   kampuni    hiyo  haitakubali   kununua  kilo   hizo    zilizozidi  upo   uwezekano  wa  wakulima   ambao  wameisha   uza   tumbaku  yao  kushindwa  kulipwa   fedha   zao  kwani   fedha   zao   zitakuwa   zimeishia  kwenye     madeni ya   pembejeo .
  Alikanusha   kuwa    viongozi wa   bodi ya   chama   hicho   haijashirikiana  na   walanguzi kuingiza  tumbaku ya  kutoka   sehemu   nyingine   bali ni  uzalishaji tuu  ndio  umeongezeka.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa