Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Mkoa wa Katavi katika kipindi cha mwaka 2015/ 2016 tafiti zinaonyesha kuwa unamaambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa kiwango cha asimlia 14 na Kitaifa maambuzi ya ugonjwa wa Malaria ni asilimia 14.8.
Hayo yalisemwa hapo jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali mstaafu Raphael Muhuga wakati alipokuwa akifungua mkutano wa mpango wa ugowaji wa vyandarua kupitia katika vituo vya kutolea huduma za Afya na katika shule za Msingi uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda uliowashirikisha wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Katavi , Wakurugenzi wa Halmashauri Waganga wakuu wa Halmashauri na Maafisa Elimu .
Alisema tafiti za mwaka 2015/ 2016 zinaonyesha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria ni asilimia 114.8 Kitaifa na Mkoa wa Katavi ni asiliimia 14 wakati kwa mwaka 2008 maambukizi yalikuwa ni asilimia 9.1 Kitaifa na katika Mkoa wa Katavi ilikuwa ni asilimia 11 ambapo kwa sasa kunaongezeko la asilimia tatu Kimkoa wa Katavi hivyo juhudi za makusudi zinahitajika ili kuweza kupunguza zaidi ya hapo .
Muhuga alieleza kuwa Serikali kupitia wadau imeanzisha mpango wa ugawaji wa vyandarua kwa jamii kupitia vituo vya kutolea huduma ya afya kwa wajawazito na watoto chini ya umri w mwaka mmoja na wanafunzi katika shule za Msingi .
Afisa mipango wa Taifa wa kudhibiti malaria Oguda Josh alisema kwa kutumia mkakati mbalimbali Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia , Wazee na Watoto ilidhamilia kuwa ifikapo mwaka 2016 maambukizi yawe yamepungua hadi asilimia tano na ifikapo mwaka 2020 maambukizi ya malaria yawe ni asilimia moja tuu.
Alifafanua kuwa mojawapo ya mkakati ya kupunguza malaria ni ugawaji wa vyandarua kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya na shule za msingi .
Lengo la mkakati huo ni kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano hivyo utumiaji wa vyandarua uliosahihi utaweza kupunguza vifo hivi kwa kiwango kikubwa sana .
Mratibu wa Malaria wa Mkoa wa Katavi Dr Benald Mbushi alieleza kuwa Mkoa wa Katavi kumekuwepo kwa ongezeko la ugonjwa huo kutokana na sababu mbalimbali .
Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni kutofanyika kwa muda mrefu kampeni za kuwahamasisha watu kudhibiti ugonjwa wa malaria kwenye maeneo yao ya kuishi na kwenye maeneo yao wanayofanyia kazi .
Pia changamoto ya miundo mbinu inayosababishwa na watu wanaochimba mashimo ya kuchimbia madini na na wanao tengeneza barabara ambao wamekuwa wakichimba mashimo na kuyaacha wazi bila kuyafukia na matokeo yake mashimo hayo yamekuwa ni sehemu ya mbu kuzaliana .
Dr Mbushi alitaja changamoto nyingine kuwa mbu siku hizi wamebadili tabia wamekuwa wakila ndani ya nyumba wanazoishi watu na kumpumzika nje ya nyumba .
0 comments:
Post a Comment