Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limewaagiza wamiliki wote wa Bar ,Grosery na sehemu nyingine zinazo uza vinywaji wahakikishe wanazingatia sheria na kanuni za sehemu ya vileo i wakati wa kipindi hiki cha sikuu ya Krismas na mwaka mpya kwa kutowahudumia vileo vya pombe watoto wote walio chini ya miaka 18.
Agizo hilo lilitolewa hapo jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damasi Nyanda alipokuwa akizungumza na Wandishi wa Habari ofisini kwake juu ya namna Mkoa wa Katavi ulivyo jipanga iliuendelee kuwa salama dhidi ya vitendo vinavyo weza kuzorotesha ustawi wa amani na utulivu wakati wa kipindi hiki cha sikukuu.
Aliwaagiza wamiliki wa bar , grosery na sehemu nyingine za kuuza vinywaji wahakikishe wanatowa huduma kwa kuzingatia kanuni za vileo kwa kuzingatia muda wa kufunga ,kuhakikisha usalama wa wateja wao na mali zao pamoja na kutowahudumia vileo vya pombe watoto walio na umri wa chini ya miaka 18
Alisema uzoefu unaonyesha kuwa kipindi kama hiki hukabiliwa na changamoto mbalimbali za matukio yanayozorotesha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kama vile kuzuka na kuongezeka kwa matukio ya uharifu ,kuongezeka kwa matukio ya ajari za barabarani ,watu kufa maji na watoto wadogo kupotea katika mazingira ya kutatanisha .
Katika kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei na kuleta athari kwa wananchi wa Katavi aliwasisitiza kila mwananchi anapaswa azingatie mambo yafuatayo ambayo aliyataja kuwa ni .
Watu wajiepushe na mazingira hatarishi wakati wa sikukuu kwa kutosherekea mbali na makazi ya watu na kutolewa pombe kupita kiasi cha kushindwa kufanya maamuzi sahihi .
Kutowaacha watoto wadogo kuzurura ovyo pasipo uangalizi ilikuepukana na ajari za barabarani na kufa maji pamoja na kupotea kwa watoto .
Aidha Kamanda Nyanda alieleza Jeshi la Polisi limejipanga vyema kuhakikisha linadumisha hali ya ulinzi na usalama katika kipindi hiki cha sikukuu kwa kufanya doria za kutambulika na za kutotambulika usiku na mchana kwenye maeneo yote yenye mikusanyiko kama vile kumbi za starehe , nyumba za ibada na kwenye maeneo yote tete yenye viashiria vya uharifu .
Alisema Jeshi la polisi litahakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa kwa mtu au kikundi chochote kitakachobainika na kukamatwa na makosa ya kuhujumu na kuzorotesha usalama katika kipindi hiki cha shamra shamra za sikukuu na kuendelea .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment