Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemwachia huru aliyekuwa Diwani wa Kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe CCM Josem Kalihosi na Mkewe Marietha Mpizi kutoka na kesi iliyokuwa ikiwakabili ya kutumiwa kukamatwa wakiwa na mikia miwili ya Tembo yenye thamani ya shilingi Milioni 45.
Kaliyosi na mkewe waliachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Mpanda hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Chiganga Ntengwa baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha ushahidi wa kuwatia hatia washitakiwa.
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Jamira Mziray alidai kuwa Kalihosi na Mkewe Marietha walitenda kosa hilo hapo Oktoba 10 2013 katika Kijiji cha Usevya ambapo kipindi hicho Kalihosi wakati huo alikuwa ni Diwani wa Kata ya Usevya CCM.
Mwanasheria wa huyo wa Serikali alidai kuwa watumiwa hao walikamatwa na askari walikuwa wakifanya operesheni ilijulikana kwa jina la tokomeza wakiwa na mikia miwili ya Tembo yenye thamani ya shilingi Milioni 45.
Mwendesha mashitaka huyo alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa walitenda kosa hilo kinyume cha sheria ya kifungu kidogo namba 86 kidogo cha kwanza na chapili na kifungu cha sheria ya uhifadhi wa wanyama pori ya mwaka 2009 na kifungu cha sheria namba 57 ya sheria ya uhujumu ya makosa ya kupanga sura ya 200 ya marekebisho ya mwaka 2002.
Akisomo hukumu ya kesi hiyo Hakimu Chiganga Ntengwa aliiambia Mahakama kuwa kutokana na mwenendo mzima wa kesi hiyo Mahakama imeona kuwa upande wa mashita umeshindwa kutowa ushahidi wa kuthibitisha kuwatia hatiani washitakiwa .
Hivyo kutoka na upande wa mashitaka kushindwa kutowa shahidi wa kuwatia hatiani watuhumiwa Mahakama imeona washitakiwa Josam Kalihosi na Marietha Mpizi hawa hatia hivyo Mahakama ya Wilaya ya Mpanda imewaachia huru .
0 comments:
Post a Comment