Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi ambayo imeongoza Kitaifa kwa matokeo ya jumla ya ufaulu wa Wanafunzi kwa 2016 waliomaliza darasa la saba kwa Manispaa zote zilizopo Nchini wamedai kuwa wataongoza tena matokeo ya ufaulu kwa mwaka 2017 kwasababu uwezo wa kufanya hivyo wanao .
Kauli hiyo ilitolewa hapo jana na Afisa Elimu wa Manispaa ya Mpanda Vicent Kayombo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye eneo la Maridadi Kata ya Majengo mkutano huo uliokuwa umeandaliwa na Diwani wa Kataya ya Majengo Willy Mbogo ambae pia ni Meya wa Manispaa ya Mpanda .
Alisema katika matokeo ya ufaulu wa Wanafunzi katika mtihani wa Taifa wa kumaliza darasa la saba kwa matokeo ya jumla yaliyotangazwa hivi karibuni Manispaa hiyo imeshika nafasi ya kwanza kwa Manispaa zote zilizopo hapa nchini.
Manispaa hiyo imeweza kushita nafasi ya kwanza kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo ambapo ilipoongoza kwa mara ya kwanza wapo watu walisema wamebahatisha na baada ya matokeo yaliofuata Halmashauri nyingi zimekuja kujifundisha kwenye Halmashauri hii.
Kayombo alieleza kuwa Manispaa ya Mpanda itaongoza tena kwa ufaulu wa wanafunzi watakao kufanya mtihani wa Taifa wa kumaliza darasa la saba.kwa mwaka 2017 kwa kuwa uwezo wa kufanya hivyo wanao kwa kuwa wazazi wapo , wadau wapo na walimu wamejipanga kufanya kazi kweli kweli .
Katika ufaulu kwa mwaka huu ufaulu wa wanafunzi katika Manispaa hiyo umekuwa ni wastani wa asilimia 96.5 na wanafunzi waliofeli ni asilimia 3.5 ambapo shule ya mwisho kwa ufaulu katika Manispaa hiyo imepata wastani wa asilimia 68 wastani ambao ni ufaulu kwa baadhi ya shule nyingine hapa nchini .
Alifafanua kuwa jumla ya wanafunzi 2116 walifanya mtihani wa Taifa wa kumaliza darasa la saba ambapo wanafunzi 2045 wamefaulu na 71 wamefeli mtihani kutokana na kuwa watoro .
Alitaja ufaulu kwa kipindi cha miaka mitatu kwa manispaa hiyo ulikuwa ni mwaka 2014 ufaulu ulikuwa ni asilimia 90 mwaka jana ufaulu ulikuwa ni Asilimia 97 na mwaka huu ni asilimia 96.5.
Alisema miaka ya nyumba watu walikuwa wanaidharau mikoa ya pembezoni kuwa haina mwamko wa elimu kitu ambacho sio kweli leo hii Mikoa hiyo iliyokuwa ikisema hivyo ndio wanaisoma namba kwa Mkoa wa Katavi ambao umeshika nafasi ya pili kwa ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba kwa matokeo ya jumla katika mikoa ya hapa nchini .
Mafanikio ya manispaa hiyo na Mkoa kufanya vizuri katika ufaulu kumetokana na mwamko wa elimu walionao wazazi na ushirikiano wanaoutowa wazazi kwa walimu pamoja na mpango kazi waliojiwekea walimu .
Nae Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo alisema Manispaa ya Mpanda imepanga kuchangisha fedha kwa ajiri ya kuboresha elimu ili wanafunzi waendelee kufanya vizuri zaidi .
Alisema kwa sasa hawana tatizo la upungufu wa madawati kwani hakuna wanafunzi wanaosoma wakiwa wamekaa chini bali tatizo lililopo ni upungufu wa vyumba vya madarasa .
Mbogo alieleza kwa sasa mkakati uliopo ni kuhakikisha nguzo zinaelekezwa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa , matundu ya vyoo na nyumba za walimu .
Pia aliwapongeza walimu wa Manispaa ya Mpanda kwa jitihada zao kubwa wanazofanya za kufundisha wanafunzi hari ambayo imepelekea kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba .
0 comments:
Post a Comment