Home » » WIZARA ya Maliasili na Utalii imeridhia maombi ya Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka ule wa kiraia

WIZARA ya Maliasili na Utalii imeridhia maombi ya Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka ule wa kiraia

 
Na  Walter Mguluchuma , Katavi .

WIZARA ya Maliasili na Utalii imeridhia maombi ya Shirika la Hifadhi
la Taifa (TANAPA) kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka ule wa kiraia
na kuwa jeshi usu ili kukabiliana na tatizo sugu la ujangili wa
wanyamapori.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya askari na wahifadhi wa shirika
hilo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi
alisema maombi ya shirika hilo kutaka kubadilishwa na kuendeshwa kwa
sheria za kijeshi ni ya msingi katika kipindi hiki ambacho Tanzania
inakabiliwa na tatizo sugu la ujangili wa wanyamapori.

Ufungaji wa mafunzo hayo ulifanyika jana  katika kambi ya Mlele ndani
ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi mkoani Katavi ambako  mameneja wahifadhi
 10 na askari  58 walihitimu mafunzo ya kijeshi ya mwezi mmoja

 “Naamini pasipo kutia shaka  mafunzo haya yatasaidia kuimarisha
nidhamu  kipindi hiki tunchojiandaa  kuingia katika mfumo tarajiwa wa
kiutendaji wa Jeshi Usu (paramilitary system)

Kwa sasa uhifadhi unakabiliwa na changamoto kubwa ya ujangili,hususan
tembo na faru kuporomoka kwa maadili ya askari na uingizaji wa mifugo
hifadhini,” alisema Meja Jenerali Milanzi.

Hata hivyo, aliwataka askari hao pamoja na Menejimenti ya Tanapa
kufanya maandalizi ya kutosha kwa msingi kuwa sheria itakapopitishwa
baadhi ya mambo yatabadilika na kuendeshwa kwa mujibu wa taratibu za
kijeshi kwa ilivyo kwa majeshi mengine nchini.

Awali akiwasilisha maombi hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan
Kijazi alisema shirika hilo baada ya kutafakari kwa kina wakitumia
wataalamu wa ndani ya shirika walibaini umuhimu wa askari wao kutumia
sheria za kijeshi kutokana na changamoto ya sasa ya katika masuala ya
uhifadhi.
 Alisema shirika  limejipanga  kuhakikisha  linakabiliana  na  hari  ya ujangili  katika  maeneo  yote .

Naye Meneja  wa Pori la  Akiba la Rukw / Lwafi , Joseph Mwang’ombe

alisema kuwa kambi  hiyo ya mafunzo  inakabiliwa na changamoto  kadhaa

 ikiwemo  uwanja wa ndege   kutokarabatiwa kwa  wakati , uchakavu wa

majengo  na miundombinu ya maji  na gharma kubwa ya uendeshaji .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa