Na Walter Mguluchuma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limepiga marufuku kwa vyama vyote vya siasa vilivyopo katika Mkoa huu kutofanya maandamano ,vikao na mikutano mpaka hapo yatakapoka maelekezo mengine kutoka jeshi la polisi kutokana hali ya usalama.
Agizo hilo lilitolewa hapo jana na Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda mbele ya wandishi wa Habari ofisini kwake katika Mtaa wa Kasimba .
Kwa mijibu wa Kamanda Damas agizo hilo ni kutokana na maandamano hayo kuwa na viashiria vya uchochezi kwa wananchi dhidi ya Serikali na kunaweza kutokea usababishaji wa uvunjifu wa amani .
Alisema Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linatowa onyo kwa mtu au kikundi cha watu kutojihusisha kwa namna yoyote ile katika kuratibu ,kuandaa ama kushiriki katika vikao ,mikutano na maandamano ya vyama vya siasa na vitendo vyovyote vile vya fujo ,ama vitisho vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani .
Kamanda Damas Nyanda alieleza Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu au kikundi chochote cha watu kitakacho kaidi igizo hilo lililotolewa na Jeshi la Polisi .
Aliwataka wananchi kuendeleza ushirikiano mwema kwa jeshi la Polisi katika kutowa taarifa za mtu ama vikundi vya aina yoyote vya watu vinavyojihusisha kuratibu na kupanga kushiriki katika vikao ,mikutano na maandamano ya vyama vya siasa yenye njama za kufanya vitendo vitakavyo pelekea uvunjifu wa amani wa aina yoyote ili hatua kali zishukuliwe dhidi yao mapema iwezekanavyo .
Aliwaomba Raia wema wenye mapenzi mema na nchi ya Tanzania ambao wanapenda hali ya ulinzi na usalama kuendelea kutamalaki waendelee kudumisha mshikamano wao kwa kutowa taarifa kwenye vyombo vya dola zitakazoweza kudhibiti vitendo vyote vya kihalifu vitakavyopelekea kuzorota kwa amani na usalama wa Mkoa wa Katavi .
0 comments:
Post a Comment