Home » » MWIGULU MCHEMBA ATAKA ASKARI WAJENGEWE NYUMBA ZA KISASA.

MWIGULU MCHEMBA ATAKA ASKARI WAJENGEWE NYUMBA ZA KISASA.


      Na  Walter   Mguluchuma .
          Katavi yetu blog
  Waziri wa  Mambo ya  Ndani ya  Nchi  Mwigulu   Mchemba ameyaagiza Majeshi ya  Polisi na  Magereza kuacha kujenga  nyumba   za  makazi ya  Askari   zenye  ramani  ya Kikoloni   na  badala yake wajenge makazi ya Askari yenye  ramani za kisasa .

  Mwigulu Mchembe  alitowa  agizo  hilo  hapo  jana  wakati  alipokuwa  akizungumza  na  askar  wa  Mkoa wa  Katavi wa  kutoka   majeshi  ya polisi , Magereza , Uhamiaji na  Zimamoto  kwenye  kikao  kilichofanyika  katika ukumbi wa  Idara ya  Maji  mjini hapa.

 Alisema  wakati Wizara ya  mambo ya  ndani   inatengeneza  Jeshi la kisasa  ni  vema  na   askari  naowakajengewa  makazi yao na yakawa ya kisasa ili yaendane  na jeshi  hilo  kuliko  ilivyo  sasa  ambapo   makazi yao yamekuwa yakijengwa kwa  ramani za toka wakati wa Wakoloni .

Mchemba  alieleza  askari wamekuwa  wakishindwa   hata kutembelewa na wazazi wao  kutokana  na  aina  ya   makazi ya  nyumba wanazoishi   .

  Hivyo    ni   vema  ramani za  makazi ya  askari  kuanzia sasa  Askari wajengewe   nyumba    ambazo  zitawaruhusu wazazi wao  kuwatembea

Alisema  tatizo la  upungufu w  nyumba za  askari  hapa   nchini  ni  kubwa  na lisipotatuliwa  linaweza kupunguza  hari  ya  utendaji wao wa  kazi  kwani mchana ukiingia kwenye  nyumba hizo  ni joto  kama   tanuli  la moto na usiku  ni  baridi

Alifafanua  kuwa  Mikoa   mpya  na  Wilaya   mpya  zinanafasi  kubwa ya kujenga  vizuri  makazi ya  nyumba za kuishi  askari kuliko  ilivyo kwa  Mikoa ya  zamani  na  Wilaya  za  zamani kwani wanayo maeneo  makubwa  .

 Aliyataka  majeshi  hayo  kuanza  kujenga  makazi  kwa kutumia  rasilimali  walizo  nazo   badala ya kukaa  wanasubilia    bajeti ya kutoka  serikalini .

 Pia  Waziri  Mchembe   aliwaeleza   askari  hao  kuwa    Polisi wanayofurusa  kubwa ya kuwasaidia watu  mbalimbali   wanaokuwa  wameonewa .

  Aidha alilipongeza jeshi la polisi Mkoani  Katavi kwa  kuulinda  Mkoa huo na kuufanya kuwa  salama  na pia kwa jitihada  zao za  kuwakamata watu  wanao hujumu  nyara za  Serikali .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa