Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog.
Mjumbe wa Kamati ya utendaji Taifa Mkoa wa Katavi wa Chama cha walimu CWT Costantine Marcely amewataka Walimu wanawake wajiendeleze kitaaluma , kiuchumi na kujishirikisha katika vyombo mbalimbali vya maamuzi katika sehemu za kazi ndani ya CWT Serikalini na kwenye taasisi nyingine .
Wito huo aliutowa hapo jana wakati alikuwa akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu Wanawake viongozi wa CWT wa kitengo cha Wanawake yaliofanyika katika ukumbi wa chama hicho na kuwashirikisha viongozi wanawake wa CWT kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi .
Alisema moja ya majukumu walionayo walimu wanawake viongozi katika sehemu zao za kazi ni kuwahimiza walimu Wanawake wajiendeleze kitaaluma , kiuchumi na kujishirikisha katika vyombo mbalimbali vyenye maamuzi sehemu ya kazi ndani ya CWT Serikalini , vyama vya siasa na kwenye taasisi nyingine .
Marcely alieleza kuwa Walimu wanawake wamekuwa hawajitozi kwenye maswala ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho kutokana na kutojiamini kuwa wanaweze hivyo ni wajibu wa walimu viongozi wanawake wakawahamasisha kugombea nafasi mbalimbali pindi zinapokuwa zimetokea .
Katibu wa CWT wa Mkoa wa Katavi Lucy Masegenya alieleza liwaeleza washiriki wa mafunzo hayo ya siku moja kuwa takwimu mbalimbali katika Sekta za elimu , ajira na uongozi zinaonyesha na kuthibitisha kwamba wanawake hawana fursa na haki sawa kama ilivyo kwa wanaume katika utoaji wa maamuzi na uwakilishi katika vyombo mbalimbali .
Alisema juhudi za shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA na vyama shirikishi kikiwemo chama cha Walimu Tanzania katika kutatua matatizo yanayowakabili Wafanyakazi zimeonyesha kuwa wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi .
Masegenya alizitaja baadhi ya changamoto kuwa ni tamaduni zilizopitwa na wakati zinazombagua mwanamke na kumnyima fursa sawa katika jamii kama vile kutorusiwa kumiliki rasilimali za familia nyinginezo .
Changamoto nyingine ni ubaguzi wa kijinsia katika ajira na fursa mbalimbali katika jamii kama vile elimu na uongozi .
Nae Mshiriki wa mafunzo hayo mwalimu Coleta Mathias alisema walimu wanawake wamekuwa wakipata wakati mgumu kuongoza kwenye maeneo ya shule kutokana na baadhi ya walimu wanaume kutokubali kuwatambua na wamekuwa wakishindwa kupata ushirikiano wa kutoka kwa walimu wenzao wa kike kutoka na tabia ya kutopendana kwa walimu wa kike kwa wakike .
Pia baadhi ya walimu wanaume wamekuwa hawapendi kukaa na walimu wa kike kwenye shule moja na matokeo yake wamekuwa wakiwafanyizia visa mbalimbali walimu wa kike .
Mwalimu Bestlila Msafiri alieleza kuwa kwenye taasisi mbalimbali ambazo wanawake wamekuwa wakipangiwa kufanya kazi baadi yao wanapopangiwa kufanya kazi maeneo ya vijijini wamekuwa wakiona hawezi kwenda kufanya kazi huko na matokeo yake wamekuwa wakitowa rushwa ya ngono ili wapangiwe vituo vya kazi za mijini.
Alieleza ilikuondokana na rushwa ya ngono ni vizuri wanapokuwa wamepangiwa kufanya kazi vijijini waache tabia ya kwenda kuomba wapangiwe vituo vya kazi vya mjini tuu wajione kuwa wanawake wanaweza kufanya kazi sehemu yoyote ile ya vijiji na mjini kwani wanawake wanaweza ,
0 comments:
Post a Comment