Home » » WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU WAOMBA KUTENGEWA ENEO LA UCHIMBAJI WALILIA NA KAMPUNI YA MZINDAKAYA

WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU WAOMBA KUTENGEWA ENEO LA UCHIMBAJI WALILIA NA KAMPUNI YA MZINDAKAYA


     Na   Walter  Mguluchuma
   Katavi
    Wachimbaji wadogo wa  dhahabu  wa  Mkoa  wa   Katavi  wameiomba   Serikali  kusiliza  kilio  chao cha  muda  mrefu   cha    kutengewa maeneo  wachimbaji  wadogo    kwa  ajiri  ya  uchimbaji  wa   madini  ya   Dhahabu .
Maombi  hayo  ya  wachimbaji  wadogo  wa  dhahabu  yalitolewa   jana  na  wachimbaji  wadogo wa  Mkoa  wa   Katavi  kwenye   Risara  yao  iliyosomwa  na   mwenyekiti wa   chama   cha    wachimbaji   wa  dogo  wa   Mkoa   wa   Katavi    Willy   Mbogo kwa   Naibu   Waziri     wa Nishati  na   Madini Dk   Medadi  Kalemani  kwenye  kikao    baina  yao  na  Naibu  Waziri  kilichofanyika   katika   Hotel  ya  Lyamba  Lyamfipa  mjini  hapa .
  Mbogo    alisema   wachimbaji  wadogo  wa  Mkoa  wa   Katavi  wanayomasikitiko  makubwa   sana  kuona  Wizara  ya  Nishati  na  Madini  imeshindwa  kufatilia  ombi  lao  la  muda   mrefu  waliloomba  kutengewa   maeneo  ya  wachimbaji wadogo wa  dhahabu katika  Mkoa  wa  Katavi  .
 Alieleza  wachimbaji  wadogo  wa  dhahabu  wa  Mkoa  wa  Katavi   hawajatengewa  eneo  la  uchimbaji  pamoja   na  maombi  yao   kadhaa  walioba  kwa  wizara  hiyo .
Eneo  wanaloliomba   wachimbaji wadogo iliwafanyie  shughuli zao     lilikuwa   linamilikwa   na  Kampuni   ya  GBA   ambalo  kwa  sasa  liko  wazi  na  lina  maombi  ya  Kampuni ya Kijani   Investment   inayomilikiwa  na  mwanasiasa  maarufu  Crisanti  Mzindakaya.
Mbogo  alisema  wachimbaji wadogo  wanazosababu za  msingi  za kuomba  wapatiwe   eneo   hilo  lililoombwa  na  Kampuni ya   Kijana   Investment kwani  mmiliki  wa  Kampuni  hiyo  ndiye   mmiliki  wa  Kampuni   za   Crystal Mkwamba ,Mkwamba   minerals, GBA     na   sasa   Kijani   Investment.
Hivyo  kampuni  hiyo  imekuwa  ikifanya ujanja  wa kubadil  majina ya Kampuni  kila  mara  na kuhodhi  maeneo  yote   yenye   mashapo  ya  dhahabu   Mkoani   Katavi toka mwaka 1998 bila  kuanzisha  mgodi  hata  mmoja  .
Alifafanua  kuwa  endapo  wachimbaji wadogo  watanyimwa   eneo  hilo wanaloliomba  na   Wizara ya  Nishati na  madini  ikampatia   mwekezaji mkubwa  atapata  tabu kuanzisha  mgodi huo  kwa  sababu ya mwingiliano  wa kuwepo na  leseni  ndogo   nyingi  kwenye  eneo hilo  hivyo  atalazimika kuwafukuza  wakazi wengi  wa eneo hilo na  huduma za  jamii zilizopo za shule  na  Zahanati  zitafungwa .
Pia  wamaiomba  Wizara  hiyo  imemalize  mgogoro  baina ya wachimbaji wadogo 32  walipewa  leseni za kuchimba  katika  eneo la  Kampuni  ambalo   eneo  hilo   jeshi  la  Wananchi wa  Tanzania  linadai kuwa  ni eneo  lao na limewasimamisha wachimbaji  hao kufanya  shughuli  kwenye  eneo  hilo licha ya kuwa na leseni  za kuchimba .
 Naibu  Waziri   Dk  kelemani  aliwaeleza  wachimbaji  hao kuwa    Wizara  inaendelea  na  mazungumzo  na  Kampuni  ya   Kijani  Investment  ilikuona   uwezekana  na   kupunguza   eneo  hilo  la  kugawiwa  wachimbaji  wadogo   na  yatari  wameisha  kaa  na  mzee  huyo  alisema   Naibu  Waziri .
  Alisema   Wzara  imepanga  kuyachukua  maeneo yote   ambayo   walikuwa  wamepewa  watu  kufanya  utafiti na  washindwa kuyaendeleza   maeneo  hayo yakisha  chukuliwa  watagawiwa   wachimbaji wagogo .
  Alisema   Kampuni  hiyo  imeomba   maneo mengi ya  uchimbaji   wakati  wachimbaji wadogo  wako   wengi  hari  hiyo  imesababisha  eneo  lililopo  kuwa   halitoshi kwa  wachimbaji wadogo .
Serikali  inatambua sana  mchango  wa  wachimbaji  wadogo   kwani  wao      ndio  huwa  ndio wanakuwa  wavumbuzi wa kwanza  wa  madini  katika   maeneo yanayopatikana  madini.
Kuhusu  mgogoro  wa  wachimbaji wagodo  na   Jeshi  la  wananchi  alisema   Serikali  itaangalia    kama  kuna  manufaa   kwa  Taifa itakayopatikana  kutokana  na  madini  yaliyopo  eneo la   Kampuni  jeshi  wanaweza  kuondolewa  kama  walivyohamisha  Gereza   Mkoani   Mbeya.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa