Home » » MAHAKAMA YA WILAYA YA MPANDA YAMWACHIA HURU LAWRENCE MASHA

MAHAKAMA YA WILAYA YA MPANDA YAMWACHIA HURU LAWRENCE MASHA


       Na   Walter   Mguluchuma  .
      Katavi yetu blog
   Mahakama  ya   Wilaya   ya    Wilaya  ya  Mpanda   imemwachia   huru   aliyekuwa  waziri wa   Mambo ya   ndani ya    Nchi   Lawrence   Masha   pamoja  na  viongozi   sita  wa   Chama  cha   Demokrasia  na   Maendeleo   CHADEMA   wa   Mkoa  wa   Katavi  baada ya   Mahakama  kuona  hawana   hatia ya  kosa  walilikuwa  wameshitakiwa  la  kuingia  kwenye   makazi ya  wakimbi ya  Katumba   bila   kuwa  na  kibali .
  Hukumu  ya  mwamwachia   Masha  na   wenzake   sita  ilitolewa  hapo  jana  na   Hakimu    Mkazi   mfawidhi  wa   Mahakama  ya   Wilaya  ya    Mpanda    Chiganga    Ntengwa  baada  ya  upande   mashitaka  uliokuwa  ukiongozwa  na  mwanasheria  wa Serikali wa  Mkoa wa  Katavi   Lungano   Mwasabila kushindwa  kutowa  ushahidi  wa  kutosha   wa  kuwatia   hatiani  washitakiwa.
  Washitakiwa   wengine  walioachiwa   huru  hapo  jana  ni   Mwenyekiti  wa   Chadema  wa  Wilaya  ya   Mpanda   Abrahamu  Mapunda  aliyekuwa  mgombea   ubunge wa  Jimbo  la  Nsimbo    chadema   ambae  pia  ni  mwandishi  maarufu  hapa   nchini   Gerald   Kitabu .  Katibu  wa   Vavicha  wa   Mkoa  wa  Katavi    Franco  Misigari ,    Mwenyekiti wa  Jimbo la   Nsimbo    Chadema   Stansilaus   Kaswele   na    katibu  wa   Jimbo   la   Nsimbo   Lameck  Costantino .
   Akisoma  hukumu  hiyo   Hakimu   Chiganga   aliiambia  Mahakama  kuwa   upande  wa  mashitaka  katika  kesi  hiyo  iliwafungulia  washitakiwa  wate   saba  mashitaka matatu ya  kuingia  kwenye  makazi  ya  wakimbizi ya   Katumba  bila  kuwa  na  kibali , pia walidaiwa  kuingia  ndani ya  makazi ya  katumba  na  bila  kibali  na  kushawishi na walishitakiwa kwa kuingia kwenye  makazi   ya  wakimbizi    bila  kibali na  kufanya  mkutano .
  Alisema  washitakiwa  ambao  walidaiwa  kutenda kosa  hilo  hapo   oktoba  20  mwaka  jana  walikana  mashitaka  hayo  kwa  kile  walichodai  kuwa    eneo  hilo  sio  kambi ya  wakimbizi  bali  ni   makazi  hivyo  hawakuwa  na  sababu  yoyote ya kuwafanya  waingie  kwenye  eneo  hilo  wakiwa   na  kibali  cha   mkuu wa  Makazi .
Aliendelea  kueleza  pamoja na upande  wa  mashitaka  kupeleka   mashidi  kumi  mahakamani  hapo  umeshindwa  kuwasilisha  kielelzo kilichoombwa  kiletwe  mahakamani na    wakili  wa upande wa  utetezi  Filbert   Msanda  kutoka  Dares   salaam  ambao walitaka waonyesha  gazeti la  Serikali  lililotangaza  kuwa  eneo  hilo  ni  la  makazi ya  Wakimbizi Hakimu  Chiganga  aliendelea  kusoma  hukumu  hiyo  kuwa  mahakama   imeona  shaka  ushahidi  uliotolewa  na   msimamizi wa  jimbo  la   uchaguzi wa  la  Nsimbo  George  Nzyungu  alidai  kuwa  yeye  alikuwa  ndiye  mwenyemamlaka ya  kutowa  kibali  cha  kuwaruhusu  chadema  kwenda  kufanya  mkutano kwenye  makazi  hayo   wakati kwa  mujibu wa   sheria   namba  16 ya  wakimbizi .
  Alieleza  mahakama   imeona  kuwa  makazi ya  wakimbizi  ya  katumba  yalianzishwa  mwaka  1973 na  makazi hayo  yalipaswa  kisheria  kutangazwa  na  gazeti la   serikali  lakini  haikufanyika  hivyo na  ya liitngazw kwa   mdomo  na  Rais.
  Hivyo  kutokana  na  kifungu  cha  sheria  namba  235  kidogo  cha   sheria   mahakama  imewachia  huru washitakiwa kuanzia  mshitakiwa  wa  kwanza  Lawrence   Masha  na  Washitakiwa  wenzake .
Akizungumzia  hukumu   hiyo   wakili  wa  washitakiwa  Filbert   Msanda    alisema  ameridhishwa  na  uamizi  uliotolewa  na   Mahakama  hiyo na  ameomba   Mahakama  nyingine  hapa  nchini   ziwe  zinatowa  hukumu kwa  haki  bila  kujali  mshitakiwa  anatoka  chama   gani  cha  siasa .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa